ONGEZA UFANISI WAKO KUPITIA VIPAUMBELE
Uwezo
wa mwanadamu unakikomo chake katika kila afanyalo. Ndio maana kuweka vipaumbele
ni jambo la msingi. Nguvu za mwanadamu ni kidogo, hawezi kufanya vizuri kila
kitu kwa wakati mmoja. Hawezi kuwekeza katika kila mradi. Hawezi kumfikia kila
mtu. Kwa kuwa pesa tulizonazo ni kidogo, muda nao hautoshi na watu tulionao
wanamajukumu mengi ndio maana tunahitaji kuweka vipaumbele.
UTAJIRI WETU KATIKA KRISTO YESU
(Waefeso1:17-23)
Biblia
imeweka wazi kwamba, watu wamjuao Mungu
wao watatenda mambo makuu. Ufunguo wa maisha yenye ufanisi upo katika
kupata maarifa, ufahamu na kujua hekima ya jinsi itupasavyo kuenenda ili kuishi
maisha ya ushindi katika Kristo Yesu. Ili kuona na kuishi ushindi katika maisha
yetu ya kila siku itategemea na kiwango cha maarifa na ufahamu wetu juu ya
“siri” za ufalme wa Mungu. Hakuna njia ya mkato katika hilo. [Mithali 4:7-9]
LINDA MAAMUZI YAKO, HASA WAKATI
UNAPOKUTANA NA CHANGAMOTO
Je
baada ya miaka mitano au kumi au baada ya muda kupita kutoka sasa, utajipongeza
kwa uamuzi uliochukua au utajilaumu? Utafurahi na kushangilia au utajutia na
kutamani kurudi nyuma ili kusahihisha uamuzi uliochukua? Kumbuka kila kitu kipo
katika uweza wa mtu mwenyewe na anawajibika kwa matokeo yote ya uchaguzi na
uamuzi wake.
FIKRA HURU KAMWE HAZIFUNGWI
Mwili
waweza kufungwa lakini fikra huru kamwe hazifungwi. Huwezi kubaki jela kama
tayari akili yako iko nje kwenye uhuru. Kuwa na fikra chanya na sahihi ni
oparesheni (brain surgery) unayoweza kuifanya mwenyewe. Ili kuwa na fikra
chanya hauhitaji kwenda hospitali ya Apollo nchini India au kule John Hopkins
Marekani , unahitaji taarifa sahihi tu. Neno la Mungu ambalo ni Habari njema
ndio taarifa sahihi. Neno la Mungu ni taa
ya miguu yetu, hutupa hekima kuliko watu wa rika letu.
PASIPO MSONGO WA MAWAZO II
(STRESS FREE
ZONE)
1.
Mpaka
lini?
Wabeba
maono wengi, watu wenye mipango ya muda mrefu na wenye shabaha za kipekee
wanaweza kuwa wahanga wa swali hili. Hili huwakumba wengi ambao wanaona umri
unakwenda, wanatamani wasimamishe saa ili watekeleze mpango kazi wao. Wana
mipango na mawazo ya kiuchumi na kijamii ambayo wanashuhudia waziwazi yakipishana na muda. Swali hili huua moyo wa Rick Warren anasema, “Hurry Kills Prayer.”
sala na kutangaza maombolezo.