Rafiki yako ni nani?
RAFIKI YAKO NI NANI?
[Aina ya marafiki ni dalili ya hatima yako]
Rafiki
ni mtu ambaye mna vitu au mwelekeo unaofanana. Rafiki ni Yule ambaye mna
mwelekeo wa pamoja katika imani, biashara au kazi. Rafiki ni yule umpendaye na
ungependa kuwa na muda mwingi pamoja naye.
Unaweza
kufanya urafiki na mtu, na cheo chake, na kitu au vitu. Urafiki na Kaizari ni
urafiki na cheo ili upate manufaa fulani,
urafiki wa Yesu na Lazaro ni mfano wa urafiki kati ya watu na upendo kati ya
Yuda Iskariote na pesa ni mfano wa watu ambao wako tayari kuwa peke yao ilmradi
wawe na pesa.
Kuna
nyimbo rafiki tunazozipenda ambazo mara nyingi tunazisikiliza, halikadhalika
kuna video rafiki, kipindi cha televisheni rafiki na hata kaseti ya redio
rafiki. Tuna kitabu rafiki tena kuna majarida na magazeti rafiki. Ukifanya
urafiki na mpumbavu lazima uumie, nyimbo za kipumbavu zinaumiza mioyo,
zinaondoa usafi wa moyo kwakuleta mawazo machafu. Biblia inasema, “Enenda pamoja na
wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.” Mithali
13:20
Kuna
nyimbo za kipumbavu ambazo ukifanyo nazo urafiki lazima uumie, kuna video za
kipumbavu, kuna vipindi vya redio vya kipumbavu halikadhalika kuna majarida na
vitabu vya kipumbavu. Kuna magazeti ya kipumbavu [udaku] rafiki wa hayo lazima
aumie. Moyo wake hautakuwa safi, utawaza uchafu wa picha ya mbele ya magazeti
hayo. Msisitizo wangu uko hapa: “Bali rafiki wa
wapumbavu ataumia.” Mithali 13:20b
Nimejikataza
kuendelea kuitazama vitu kwenye “you tube”
kwani picha za matangazo na picha chafu zinazowekwa makusudi zimekuwa kama
mtego kwangu. Kuliko kumkosea Mungu kila siku ni bora nisiingie kabisa. Kila
mtu ana eneo lake analojaribiwa kwalo, wengine ni urafiki na magazeti, wengine
mitandaoni, wengine mavazi na wengine mazungumzo mabaya. Wengine hujaribiwa kwa
kutaka kuvutia au kupendwa na watu, hawa huweka picha za mtego wakitegemea
aonaye awape, “like” au awakubali.
Rafiki
ni yule anayezungumza nawe, magazeti, vitabu, majarida na picha huzungumza nasi.
Lengo la mwandishi ni kuona msomajia ua mtazamaji anapata ujumbe kusudiwa. Mara
nyingi huwa sitazami wala kusikia nyimbo za kidunia [kipumbavu] lakini huwa
inanilazimu nikiwa safarini. Nyimbo hizo hupigwa ndani ya basi na madhara yake
ni hasi. Huwa nasafiri nikiwa na vitabu na majarida mazuri ya kusoma lakini
bado kwa masaa kumi na nne au kumi ya safari nyimbo za kipumbavu huleta kero na
uchafuzi wa moyo. Kama watu watapata ajali huku wakitazama nyimbo chafu basi
mioyo yao itakuwa katika hali mbaya.
Tunaweza
kujaribiwa kwa kuwa na makundi yenye mazungumzo mabaya lakini kwa kuwa na tabia
ya kuchagua vitu vinachochea tamaa mbaya. Ni muda mzuri leo wa kuamua kuacha
kabisa urafiki na kipindi kichafu cha redio au televisheni, ni muda mzuri wa
kuvunja urafiki mbaya. Rafiki mpumbavu atafanya uangamie, napenda tafsiri hii:
“The companion of fools will suffer harm”
Mfano
mzuri wa madhara yanayompata rafiki wa mpumbavu ni yale ya nchi ya Japani
iliyoyapata kutoka Marekani kufuatia urafiki wao na Hiltrer wa Ujerumani.
Japani walifanya urafiki na Ujerumani kwa kusaini mkataba wa ulinzi na usalama
wa mwaka 1940 matokeo yake mbeleni walivamia kisiwa kimoja nchini marekani na
kuambulia kupigwa mabomu ambayo mpaka sasa wanayaonja madhara yake. Yote hayo
ni kwa sababu ya rafiki mpumbavu. Nakushauri achana naye na kesho yako itakuwa
njema.
0 comments :