Kuelekea Uhuru wa Kifedha - II
KUELEKEA UHURU WA
KIFEDHA II
(THE BIBLICAL LAWS OF MONEY)
Toleo lililopita tuliangazia kanuni moja
muhimu sana ili kuelekea mafanikio ya kiuchumi katika maisha ya mtu; kanuni ya
uzalishaji bidhaa au huduma. Kanuni hii huwa haimzungumziwi sana lakini ni kanuni
muhimu sana kuelekea uhuru wa kifedha. Kumbuka, Fedha unazozitafuta zipo kwa watu, ili kuzipata lazima uwe na kitu cha
kubadillishana (exchange). Hakuna namna utafikia uhuru wa kifedha endapo
hakuna bidhaa wala huduma ambayo unaweza kutoa na watu wakakupa fedha.
Kwa mtu ambaye ameajiriwa maana yake anauza
huduma, na hivyo mwisho analipwa mshahara. Mshahara unakuja kama matokeo baada
ya kutoa huduma, vivyo hivyo mfanyabiashara au mjasiriamali au hata makampuni
hupata fedha kutokana na bidhaa au huduma wanayozalisha. Fedha ni matokeo ya bidhaa au
huduma anayotoa mtu. Mwalimu wangu mmoja amewahi kusema, “If you don’t create or add value to others
(through goods or service), you are not entitled to receive money” (Kama
hauna bidhaa au huduma unayoweza kutoa kwa watu, haustahili kupokea fedha ya
mtu: Tafsiri isiyo rasmi)
Mtu pekee anayeweza kuwa na uhakika wa
kupata fedha bila kubadilishana na huduma au bidhaa moja kwa moja ni serikali,
yenyewe inakusanya kodi. Hivyo watu watake au wasitake ni lazima serikali
ikusanye fedha kutoka kwao kama kodi kwa mujibu wa sheria za nchi husika. Mimi
na wewe hatukusanyi kodi, watu hawalazimiki kisheria kutupa fedha zao; hivyo
basi ili kupata fedha zao lazima tuwe na kitu wanachokiitaji na kwa sababu hiyo
wako tayari kukilipia ili kukipata kitu hicho. Na hapo ndipo tunapoweza kuona
fedha inaingia mifukoni mwetu.
Swali unaloweza kujiuliza au unalotakiwa
kujiuliza sasa, ni bidhaa gani au huduma gani unaweza kuizalisha au kutoa
ambayo watu (jamii inayokuzunguka) wanahaja nayo na watakuwa tayari kuilipia
ili kuipata? Iwe umeajiriwa au hujaajiriwa hili ni swali muhimu sana kama
unataka kufikia uhuru wa kifedha (kutimiza mahitaji yako YOTE, na kupata ziada
kwa ajili ya kufikia mahitaji mengine yanayokuzunguka; maana utamsaidiaje
anayehitaji ‘chakula’ wakati hata wewe huna: Mathayo 25:37-40).
Sam Adeyemi amewahi kusema “It is
not the absence of money that makes a person poor; it’s the absence of right
idea (thought) that has value”. Yaani “Si ukosefu wa fedha ndio humfanya
mtu kuwa masikini bali ukosefu wa wazo lenye thamani”. Hivyo kumbe fedha ni
matokeo tu; yaani matokeo ya wazo lenye
thamani ambalo huzaa bidhaa au huduma; ambazo mtu hubadilishana (exchange) na
fedha.
There’s a place for you at the top!
0 comments :