Umuhimu wa kutambua kusudi - I
Umezaliwa ili kufanikisha jambo mahususi katika maisha yako. Kuzaliwa kwako ni jibu la Mungu juu ya uhitaji ulipo katika kizazi chako. Kazi kubwa ya kwanza ulionayo ni kutambua jambo hilo ndipo uweze kuishi kwa ufanisi. Tafiti mbali mbali zinaonesha, watu waliofanya mambo makuu duniani, ndani ya mioyo yao walishawishika na ukweli huu, ya kwamba wameumbwa kwa ajili ya kufanikisha jambo fulani mahususi. Jambo hilo ndilo huitwa kusudi la kuzaliwa kwako.
Kusudi maana
yake ni sababu iliyofanya au inayofanya kilichopo kiwepo au kitengenezwe jinsi
kilivyo ili kutimiza kazi maalumu katika kufikia malengo yaliyokuwa
yamekusudiwa awali kabla ya kitu hicho kuwepo au kutengenezwa. Kutambua
sababu ya kuwepo kwako ni jambo la msingi kuliko yote unayoweza kufanya.
Ile
kwamba kila kitu kimeumbwa kwa kusudi maalumu haina maana kwamba kila kitu
kinaishi kulingana na kusudi hilo la kuwepo kwake. Kumbuka jambo hili: Tumepewa
muda wa kuishi; hatujapewa muda wa majaribio ya kuishi. Ni hasara kwa mtu
kukutwa na mauti wakati bado yupo kwenye majaribio ya kuishi.
Kwanini
kutambua kusudi la Mungu juu ya maisha yako ni jambo muhimu:
- Kusudi ndilo linalokupa kujua sababu ya kuumbwa kwako. Ni hasara kwa mtu kufanya kila kitu katika maisha yake isipokuwa kufanya alichokusudiwa kufanya.
- Kusudi ndio chanzo cha utoshelevu wa kweli katika maisha ya mtu (sense of fulfillment).
- Kusudi hutupa msukumo na ujasiri wa kusonga mbele katika maisha yetu ya kila siku bila ya kukwamisha na changamoto zinazojitokeza.
- Kusudi linakupa uhakika juu ya maisha yako ya kesho leo. Na hivyo hukupa msingi imara ya Imani isiyoweza kuyumbishwa na kitu chochote. Kukupa uhakika juu ya mambo yatarajiwayo. [Habakuki 2:3-4]
- Mungu hufanya kazi kwa kuliangalia/kuzingatia kusudi lake. [Waefeso 1:11].
- Mungu hufanya kazi kwa kuhakikisha kusudi lake linatimia (He is committed to His purposes) Isaya 14:24
- Unapotambua kusudi, hofu hutoweka. Unapotambua ulipokusudiwa kwenda inakupa kujua kuwa ulipo sasa ni kwa kitambo tu. When you know where you are going, where you are becomes an adventure. [Zaburi 23:3-5]
Hizo
ni baadhi ya sababu kwanini kutambua kusudi la Mungu katika maisha yetu ni
muhimu. Ikiwa Mungu hufanya kazi kwa kuhakikisha kusudi lake linatimia, hii
inatupa uhakika na ujasiri wa kutembea katika mafanikio ya kweli siku zote kwa kuwa Mungu anakuwa upande wetu ili
kutufanikisha.
Kabla ya Mungu kukufunulia kusudi
lake kwa maisha yako, Hujifunua kwako kwanzo; Hukukutanisha na U-Mungu wake. Ndio
maana kumpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako ni Muhimu, si tu kwa
ajili ya kwenda Mbinguni lakini pia unapata fursa ya kutambua kusudi la Mungu
kwako na kukuwezesha kuishi maisha yenye ufanisi na mafanikio ya kweli.
See you at the top
0 comments :