Unataka kufanikiwa katika nini - II?
UNATAKA KUFANIKIWA KATIKA NINI - II?
“Success is predictable, so is the
failure”
Kiwango cha
mafanikio ya mtu katike eneo lolote hutegemea kiwango chake cha maarifa sahihi,
ufahamu na utendaji kazi wa kanuni zinazoleta mafanikio katika eneo
hilo. Toleo la kwanza katika mfululizo huu tuliangalia kanuni/ mambo mawili; Na
leo nataka tuangalie mambo mengine mawili:
a. Je, unaona au unaliona (ndani yako) jambo
hilo unalotaka kufanikiwa au kufanikisha (Do you see it)?
Mpaka umeliona
jambo hilo waziwazi ndani yako, hautaweza kulimiliki/ kulifanya kuwa dhahiri.
Kwa kadri unavyoona ndivyo unavyoongeza eneo la umiliki wako yaani uwezekano wa
kulifanikisha jambo hilo au kufanikiwa katika eneo hilo. “Maana nchi hii yote uionayo,
nitakupa wewe na uzao wako hata milele”. Kipimo cha Ibrahimu hakikuwa kwa
Mungu aliyeahidi, kilikuwa katika uwezo wa macho yake kuona. Mungu hakumuwekea
mipaka; mipaka iliwekwa na macho yake. “Inua macho yako ukatazame
kutoka hapo ulipo”. (Mwanzo 13:14-15, 17)
Ukitazama
kutoka hapo ulipo (ambapo unachotamani na
kutaka kufanikisha kipo kama wazo tu kwenye maandishi/mchoro) unaiona hiyo
nchi? Je unajua ya kuwa unajua ya kuwa unaweza kufanikiwa au kufanikisha jambo
hilo uliloliandika? Kuandika ni jambo moja, na kujua ndani yako kuwa unaweza (confidence) kufanikiwa/kufanikisha ni
jambo lingine. Kumbuka, tunapewa au
tunapata kile tunachokiona. Habakuki aliambia, “Ukaifanye kuwa wazi
sana…” Mpaka macho yako yameona (wazi wazi) kwanza, hautaweza kumiliki
kikamilifu. Kwa kadri unavyoona vizuri ndivyo unavyoweza kutembea kwa kasi
kufikia mafanikio yako (The more clearer you can see it, the greater the
speed of delivery).
Warren Baffett,
anasema kabla hajawa tajiri aliona (he saw it clearly) atakuwa tajiri,
wala hakuwa na shaka hata dakika moja. “I always knew I was going to be
rich. I don’t think I ever doubted it for a minute.” –(“Siku zote nilijua
kuwa, nitakuwa tajiri. Sidhani kama nimewahi kuwa na mashaka juu ya hilo (ndani
yangu) hata kwa dakika moja”: Tafasiri isiyo rasmi). Mwanadada Emma Wenani
anasema, “Deep down, I always knew I would be successful” (“Ndani kabisa
ya moyo wangu, nilikuwa najua nitafanikiwa”: Tafasiri isiyo rasmi). Ndani ya
moyo wako unaona nini? Unachoona ni muhimu sana, kwa sababu kinaweza
kukukwamisha au kukufanikisha.
b.
Tafuta maarifa,
elimu na ufahamu wa ‘kutosha kuanza’
jambo hilo/ kuhusu eneo
Kabla ya kuanza
jambo lolote lenye maana, ni muhimu kuwekeza katika kupata maarifa sahihi
na ufahamu wa kutosha kukusaidia kuanza. Kiwango chako cha mafanikio katika
eneo lolote hutegemea kiwango chako cha maarifa na ufahamu uliona nao kuhusu
eneo/jambo hilo; iwe kiroho, kimwili, kifedha au kiuchumi, familia, huduma,
mradi, uwekezaji n.k. Unapopata maarifa sahihi ya kukuwezesha kuanza matokeo
huwa dhahiri. Mfano. Usianze mahusiano, au ndoa, biashara, kilimo, mradi au
uwekezaji wowote ule kama huna maaarifa sahihi na ufahamu wa kukusaidia kuanza
vyema; Don’t start blindly. Hili litakuepusha na msongo wa mawazo (stresses and depressions)
pamoja na gharama nyingine nyingi sana kama vile muda, fedha n.k. Ukianza bila
kuwa na maarifa na ufahamu wa kutosha uwe na uhakika jambo hilo halifiki mbali
au litakugharimu sana. Kumbuka, Mpaka akili imetoka jasho, hautaweza kuona wepesi
(Until your brain sweat; you won’t experience swiftness).
Japo kujifunza
ni jambo endelevu, lakini ni muhimu kuhakikisha kabla ya kuanza jambo lolote
unapata maarifa yaliyo sahihi yatakayokusaidia kuanza vyema.
Unataka kuona wepesi katika ndoa, uhusiano, huduma, biashara, kilimo, mradi au
uwekezaji wowote ule? “Yale uliyoyaona kwa macho, usitoke nje kwa haraka ili
kuyashindania; usije ukakosa kujua la kutenda hatimaye...” (Mithali 25:7c-8)
There’s a place
for you at the top!
0 comments :