Je hamkusoma?
JE, HAMKUSOMA?
(Mathayo 19:4-6)
Matatizo mengi katika maisha ya mwanadamu
ni matokeo ya semina alizokataa kwenda na vitabu alivyokataa kusoma. Askofu
David Oyadepo anasema, “Kabla hujaoa au kuolewa jitahidi angalau (at least) usome vitabu (50) hamsini kuhusu
mambo ya mahusiano na ndoa”. Ni wachungaji wachache wako tayari kuusema ukweli
huu mchungu, matatizo ya ndoa ni matatizo ya maarifa.
Kuna nyakati mchungaji wetu mkuu yaani,
Yesu Kristo alihojiwa kuhusu matatizo ya ndoa, naye bila kumumunya maneno alisema,
ni matatizo ya kutokusoma. Aliwajibu akawaambia, “….Hamkusoma ya kwamba….”
Mathayo 19:4
Wangesoma wangejua. Atakachofanya shetani
si kukuzuia usiolewe, bali atakuzuia usisome. Mafundisho ya wiki mbili, mwezi
mmoja au mwaka mmoja hayawezi kusaidia, ni lazima usome. Talaka, ugomvi, watoto
wa mtaani na jamii zisizo na maadili zote zinasababishwa na jambo moja, ukosefu
wa maarifa. Nikiwa chuo kikuu mzumbe nilimweleza rafiki mmoja, kama hauko
tayari kusoma hauko tayari kuishi.
Sasa unaweza ukaelewa kwa nini watu wana
wake wengi, sasa unaweza ukaelewa kwa nini watu wana waume wengi, sasa unaweza
ukaelewa kwa nini makanisa ya leo yameanza kuongeza muda wa mafundisho. Ni kwa
sababu ya ukosefu wa maarifa, hawakusoma!
Hakuna familia bila msamaha, hakuna ustawi
kama familia itakuwa kipaumbele cha pili. Kuna ndoa za kibudha, ziko za
ki-mila, na ziko za kiserikali. Kila hiyo inakanuni na taratibu zake, lakini ni
zile zinazofungwa kwa mtazamo wa falsafa ya Yesu Kristo ndizo zitakazo weza
kuleta maana kwa dunia hii. Ni familia hizo ndizo zitaleta ufalme, watoto
watakao mtisha shetani badala ya kumwogopa, watoto watakao tumia ustadi na
akili zao kwa maendeleo ya kudumu ya jamii zao. Si tu kwamba umezaa mtoto bali
umemzalia nani, Mungu au shetani, mbingu au Jehanamu?
Bila ya mama, ni bila ya upendo; na bila ya
baba, ni bila ya ulinzi, vyote havikuachi salama. Nimewasikiliza wachungaji
zaidi ya 8 katika jambo hilo wote wanasema mambo haya kwa pamoja; 1. Uzuri au
utanashati unadanganya bali chagua mtu amchaye BWANA, 2. Usioe kabla hujajua
makusudi ya kuumbwa kwako, 3. Kazi kwanza ndoa baadaye yaani, usiolewe na mtu
asiyejituma kufanya kazi hata ndogo ndogo, 4. Usioe nje ya kanisa, zamani watu
walirudi kwao sasa hivi ni kanisani yaani, mtu aliyemwamini Kristo na kuokoka,
5. Usiwe na haraka, “don’t rush”, 6.
Usipuuze ushauri wa jamii kuhusa ushuhuda wa huyo mtu, 7. Fuata sifa
ulizojiwekea na si umbo na muonekano, review
your checklist, 8. Oa chagua la Mungu na si chagua lako.
Nilisikia kwa Benny Hinn na Sunday Adelaja
wakisema, “Mary God’s choice and not your
choice” yaani “uungane na mtu ambaye Mungu amekuchagulia na si ambaye wewe
umemchagua”. Hii hupelekea mtu kuomba sana na kusoma sana. Katika maombi Mungu
atakuongoza, na katika neno Mungu atakuangazia, kwa kuwa neno ni taa. Taa
ikiangaza ni rahisi kuona na kuwa na hakika na salama.
Kwa muhtasari, soma kabla ya kuingia katika
uhusiano, lijue kusudi la kuumbwa kwako kabla ya kuingia kwenye uhusiano.
Unaweza pia kuagiza kitabu cha, “Si kwa
tamaa, bali kwa upendo” ni kizuri na kinapatikana kwa namba zetu.
Barikiwa….
0 comments :