Unataka kufanikiwa katika nini - III
UNATAKA KUFANIKIWA KATIKA NINI - III
“Success is predictable, so is the failure”
Unatumiaje muda wako wa ziada?
Moja ya jambo kuu linalotofautisha kati ya
mtu aliyefanikiwa na watu wengine, ni namna wanavyotumia muda wao wa ziada.
Mwenye hekima mmoja amewahi kusema, namna unavyotumia muda wako leo ndio uamua
hatima yako ya kesho. Nioneshe unavyotumia muda wako wa siku, nikueleze hatima
yako. Wote tuna masaa 24, wote tunamahitaji ya msingi yanayohitaji muda mfano.
Kulala, kula, kusoma (darasani kwa mwanafunzi), kufanya kazi n.k, lakini swali
langu la msingi kwako ni je unatumaije muda wako wa ziada?
Muda ni kitu cha ajabu sana, ukichagua
kuutumia vizuri au kutoutumia kabisa, bado muda utapita. Ukiamua kulala siku
nzima, muda hautasimama, chochote utakachoamua kufanya bado muda utapita; ukiamua
kukaa tu bila kufanya chochote bado muda utapita; hata ukiamua kuvunja saa bado
muda utapita. Hivyo ni muhimu kuzingatia namna tunavyotumia muda wetu. Kumbuka
hauwezi kuhifadhi muda kwa ajili ya matumizi ya baadae.
Leo nitagusia aina mbili za watu linapokuja
swala la muda; kuna watu wanaopoteza muda na kuna watu wanaowekeza muda. Hivyo
kila muda unaopita katika maisha yako, unakuwa umewekezwa au umepotezwa. Kitu
kinachoamua kama umepoteza au umewekeza muda wako ni namna unavyoutumia muda
huo. Katika mahojiano yake na jarida maarufu la nchini Marekani, Dr. David
Oyedepo aliulizwa, unatumiaje muda wako wa ziada, akajibu “I use my time to read and think” yaani natumia muda wangu kusoma na
kutafakari (personal development).
Wewe na mimi tunatumiaje muda wa ziada?
Mfano; Ukisafiri umbali mrefu unafanya
nini, unalala muda wote mpaka unafika? Unaangalia filamu na muziki wanaokuwekea
mpaka unafika?!!!! Kwanini usibebe kitabu uwe unasoma wakati wengine wamelala?
Kwanini usiweke mafundisho ya sauti kwenye simu yako ukiwa na spika za
masikioni (earphones) wakati wengine wanasikiliza bolingo? Nina uhakika mpaka
unafika mwisho wa safari yako utakuwa umemaliza sura mbili hadi nne za kitabu;
na hapo tunasema umewekeza muda wako.
Au ukiwa kwenye foleni za mjini na umepata
kiti cha kukaa, unafanya nini? Unalalamika kuhusu foleni mpaka unafika?
Unachati mpaka unafika? Unalala? Au unatumia muda huo kujifunza ili uwe bora
zaidi katika eneo unalotaka ufanikiwe? Embu tufikiri pamoja, mtu anayekaa
kwenye foleni saa moja au mawili au zaidi kwa siku na kuishia kulalamikia
foleni na serikali au kuchati, na mtu mwingine anatumia muda huo kujifunza
(kitabu au mafundisho ya sauti kwenye CD kwa gari binafsi) namna ya kuwekeza
katika biashara au ujasilimali au uwekezaji jambo lolote hata familia, huduma
au kazini; unafikiri baada ya mwezi mmoja watu hawa watakuwa sawa kifikra?
Baada ya miezi sita watakuwa sawa kimaisha? Au ukiwa nyumbani unatumiaje muda
wako? Kumbuka: Nioneshe unavyotumia muda
wako, nikuoneshe hatima yako…. Wito wangu kwako leo ni kwamba, Anza kuangalia
namna unavyotumia muda wako; tumia muda wako kuwekeza katika kuongeza ubora
kwako binafsi (personal development)
au kuongeza ubora katika eneo unalotaka kuona mabadiliko na mafanikio.
There’s a
place at the top
0 comments :