Unataka kufanikiwa katika nini?

1:00:00 PM Unknown 0 Comments


UNATAKA KUFANIKIWA KATIKA NINI?
“Success is predictable, so is the failure”
Nakubaliana na mwenyehekima mmoja aliyesema, “Success is predictable, so is the failure” (“Kufanikiwa au kutofanikiwa ni jambo la kutabirika”: Tafasiri isiyo rasmi). Kwa lugha rahisi ni kwamba mtu anaweza kujua kama atafanikiwa au hatofanikiwa katika maisha yake au katika jambo fulani kabla hata hajaanza safari. Mara nyingi nmeandika kuwa “Mafanikio katika jambo lolote kwenye maisha ya mtu si jambo la bahati nasibu; mafanikio huja baada ya kufuata na kutekeleza kanuni muhimu katika maisha ya mtu”. Na hiki ndicho kinachofanya mafaniko katika eneo lolote kuwa ya kutabirika (predictable) kwa kuwa mafanikio yamefungwa ndani ya kanuni (universal principles/laws).
“I always knew I was going to be rich. I don’t think I ever doubted it for a minute.” - Warren Buffett
(“Siku zote nilijua kuwa, nitakuwa tajiri. Sidhani kama nimewahi kuwa na shaka juu ya hili hata kwa dakika moja”: Tafasiri isiyo rasmi)
Kiwango cha mafanikio ya mtu katike eneo fulani hutegemea kiwango chake cha maarifa na ufahamu juu ya kanuni za mafanikio katika eneo hilo; iwe kiroho, kimwili, kifedha au kiuchumi, familia, huduma n.k (Mithali24:3-5). Leo nataka tuangalie kanuni/mambo mawili:
a.    Ufasaha wa maeneo unayotaka kufanikiwa au mambo unayotaka kufanikisha (clarity of vision)
Maisha ya kila siku yanadai mtu awe na uwezo wa kujua kwa ufasaha (clarity) anataka afanikiwe katika jambo gani ili kuishi maisha yenye kuleta matokeo (productive / effective life). Je, umeshawahi kukaa chini na kujiuliza unataka kufanikiwa katika nini kwenye maisha yao? Au unataka kufanikisha nini katika muda wa kuwepo kwako hapa duniani? Nakushauri tafuta muda ujiulize na kupata majibu ya maswali hayo. Tunaishi katika ulimwengu ambao kila mtu anaonekana kuwa ‘bize’, lakini ni watu wachache wanaoweza kuonesha matunda au matokeo ya ‘ubize’ wao; kwa watu wengi hasa vijana, ni rahisi sana kuwa ‘bize’; lakini si rahisi kuonesha matunda ya ‘ubize’ wako. Kusema tu unataka ufanikiwe katika maisha haitoshi, lazima uwe ‘specific’ ili uweze kujipima na kujitathimini kulingana na muda.
b.   Iandike njozi hii
Mambo mengi yanadai umakini wetu, muda wetu na rasilimali zetu; ndio maana kama hatua ya kwanza, tunahitaji kutambua (Define clearly) maeneo au mambo tunayotaka kuyafanikisha na kuyaandika mambo hayo sehemu maalumu itakayokuwa rahisi kwa kuyaona mara kwa mara. Kutambua pekee haitoshi, jifunze kuandika mahali. Labda unataka kuandika kitabu au kuanzisha biashara au kuanzisha chanzo kipya cha mapato au mradi (project); hata kama mazingira hayafanani na kile unachotaka kufanikisha fuata ushauri aliopewa Habakuki, Iandike (Hab 2:2); unapoandika wazo lolote linakuwa wazi zaidi (clarified) ndani yako na inakupa hamasa na wepesi wa kuliendea. Kwa utafiti mdogo tu, asilimia kubwa ya watu waliofanikiwa katika maeneo mbalimbali; walikuwa na mawazo hayo ya vitu au mambo tunayoyaona kwao wakati huu kwenye maandishi, waliandika matamanio yao; waliyaona na kuyaandika kabla ya sisi kuyashuhudia...!
There’s a place for you at the top!

0 comments :