Kupatwa kwa jua

3:08:00 PM Unknown 0 Comments

KUPATWA KWA JUA.
(Wafu hawawezi kumchagua Yesu wala kumkataa shetani)
Alhamisi, Septemba Mosi ilikuwa siku ya kupatwa kwa jua. Maeneo mengi ya mkoa wa Mbeya hususani Rujewa yalishuhudia kufifia kwa mwanga na giza kutokea kwa masaa kadhaa. Naamini ilikuwa hivyo kwa maeneo mengi ya Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Kituo cha habari cha BBC kilifanya mahojiano na Mheshimiwa Ghalib Bilal kuhusu kupatwa kwa jua na hapo nikataka kusikia machache kuhusu jambo hilo. Katika mahojiano hayo dondoo kubwa niliyopata ni kwamba, “kupatwa kamili hutokea mara moja katika eneo fulani kila baada ya miaka 300.” Kupatwa kamili kwa jua kutatokea tena hapa nchini kwetu miaka 360 ijayo. (At any place on Earth, a Total Solar Eclipse can be seen on average once every 360 years.). Only my grave will witness that.
Miaka mia tatu ijayo mimi wala wewe hatutakuwepo. Kumbe hatuna nafasi ya kuona tena kupatwa kamili kwa jua tukiwa Tanzania. Tunachoweza kukiona tena ni kupatwa kwa kawaida tu ambako hutokea mara kwa mara na si kupatwa kamili. Je, utakuwa wapi miaka mia tatu ijayo? Je, ratiba yako ya siku inakupa kujiandaa na maisha hayo ya umilele?
Ni vema kujiandaa! Ni ukweli ulio wazi, dhambi ni kikwazo cha maandalizi yetu. Kama ilivyokuwa kwa Adamu watu hawatendi dhambi kwa bahati mbaya au kwa kudanganywa, bali hutenda kwa kuchagua. Yesu alikuwa kijana na alijaribiwa kama sisi na hakutenda dhambi. Dhambi ni uchaguzi. Tunatenda kwa sababu tumeamua kumkana na tumechagua kutenda. We sin not because we have to, but it is because we want to.
Kila siku watu zaidi ya mia moja hamsini hufariki, magaidi nao wanasababisha vifo katika halaiki za watu. Kuuawa na gaidi hakukufanyi uokoke, unamuhitaji Yesu kwa umilele wako. Mamia ya wanachuo wa Garisa huko Kenya waliuawa na magaidi wa alshababu; tukio hilo haliwapi marehemu hao kumwona Mungu ikiwa hawakumchagua Yesu wakati wa uhai wao.
Ukimkataa Yesu ukiwa hai huwezi kumkubali ukiwa kaburini, ndio maana hakuna nchi duniani ambayo marehemu wanapiga kura. Wafu hawawezi kumchagua Yesu wala kumkataa shetani. Ni walio hai tu ndio wana uwezo huo. Dereva mmoja akielezea uzoefu wake wa kesi za ajali za barabarani alisema, “Marehemu hashindi kesi.”
Ukikosa kufika mbinguni huwezi kukosa kufika motoni. Wasio kwenda mbinguni huenda motoni. Watu wengi hawavutiwi sana na kwenda mbinguni kwa sababu hakuna walichowekeza huko. Hawajawekeza tumaini, imani, upendo, fedha wala matendo mema; hakuna wanachotazamia kukiona wakifika huko, ndio maana hawana fikra za kwenda huko.
Donald Trump anapokwenda Uingereza anakwenda kuona alichowekeza, Dangote anapokuja Tanzania (Mtwara) ni kutazama alichowekeza huko. Tukiweka pesa zetu mbinguni, tukikataa mambo ya dunia basi bila shaka shauku yetu ya kwenda mbinguni itaongezeka mara dufu maana tumewekeza huko. Hakuna mfanyabiashara anayeridhika kwa kupata taarifa za simu tu bila ya kufika eneo ilipo biashara yake ilikujiona kwa macho kinachoendelea, vivyo hivyo haitoshi kusikia tu simulizi za mbinguni ni lazima siku moja tufike huko.
Yesu alikuja kwa sababu ya walio wake, na sisi hatuna budi kumfuata aliko kwa sababu Yesu ni wetu. Tukiwekeza hazina yetu mbinguni tutatamani kwenda kwa sababu hazina ya mtu ilipo na moyo wake upo. Jifunze huduma kama hawa wa Luka 8:3 ambao waliamua kuhubiri na Yesu kwa fedha zao: “na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao.
BWANA AKUBARIKI

0 comments :