Usioneshe kama hutaki kuigwa
(Don’t show it if you don’t want to be imitated)
Watu
wengi wanaonesha mambo ingawa nia yao ya ndani hawataki watu wengine wayaige
mambo hayo. Katika mchezo wa mieleka (WWE) baada ya kuonesha matangazo ambayo si salama kwa
watoto eti wanasema, usijaribu nyumbani, “Don’t
try this at home.” Ubongo wa mtu humuamuru kutenda na kutendea kazi kile
akionacho.
Wale
wa sigara nao baada ya kuandika mandishi makubwa yenye kusisitiza uongo, na
kuweka vibwagizo vyenye kuonesha sigara ilivyotamu kama vile, “ni tamu, ni fresh,
ni yako” ndipo wanaweka maandishi mengine madogo yasemayo, “uvutaji wa sigara
ni hatari kwa maisha yako.” Wanasisitiza uongo kwa herufi kubwa na ukweli kwa
herufi ndogo kabisa, mwandishi amefanya tofauti kidogo katika makala hii ili
kukemea uvutaji wa sigari ambao kimsingi huleta saratani na magonjwa ya kifua.
Unadhani
ni kwa nini makampuni yanawekeza mamilioni ya fedha katika matangazo? Fikiri ni
kwa nini wasanii wanaofanya matangazo hayo hulipwa maradufu? Hivi karibuni hapa Tanzania kampuni moja ya
simu imeshindwa kuendelea kumlipa msaanii mmoja aliyedai kuongezewa pesa kwa
ajili ya matangazo ya biashara anayoyafanya na kampuni hiyo. Jawabu ni moja
makampuni yanaamini watu wakiona wanaamini, na huo ndio ukweli. Kampuni
zinapata wateja lukuki kupitia matangazo kwa kuwa kile wateja waonacho huamini
na kufanya.
Kila
fainali za kombe la dunia zinapoisha vijana huanza tabia na mitindo mpya toka
kwa wechezaji. Ukitazama mitindo yao ya kunyoa nywele na mavazi utajifunza
kitu. Kuna nguvu katika kile walichokiona. Ukitambua hili utaona umuhimu wa
kuonesha yale tu unayotaka yaigwe. Haijialishi ni mavazi, picha, matendo au
maneno tusemayo. Ni vema tusema mambo ya kuigwa, tuishi kwa kuigwa na tuvae kwa
kuigwa. Don’t show it if you don’t want
to be imitated!
Si
lazima watu waokolewe kwa kusoma neno na kuhubiriwa, wakati mwingine waokolewe
kupitia mienendo yetu. Biblia inasema kuna nyakati unaweza kuoa au kuolewa na
mtu asiye amini (mpagani) na kupitia wewe (matendo na maisha yako) atakayo
tazama anaweza kuokoka. Kuna nguvu katika kile unachoona. No one in the bible had the bible.
Usitazame
kile usichotaka kuwa. Nilimuulize mtoto mmoja anayetazama mieleka kwamba,
unampango wa kupigana? Akasema, “Hapana, ila mtu akinichokoza nampiga za
hivyo.” Somo hapa ni kwamba, ukitazama sana visivyofaa utatenda isivyofaa
pia.
Rai
yangu kwako, usione visivyofaa wala usioneshe usichotaka watu waige.
0 comments :