Chagua Heshima

4:07:00 PM Unknown 0 Comments


CHAGUA HESHIMA

Jitahidi uwe chombo cha dhahabu

Watu wengi wanapata heshima katika jamiii kwa sababu mbalimbali ambazo huhusisha pia mafanikio yao. Lakini si wote wanaoheshimiwa na wanadamu huheshimiwa na Mungu pia. Watu wengi tunapata heshima ya wanadamu huku tukikosa heshima mbele za Mungu. Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina. Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema.”  2Timotheo 2:20-21
Mungu akikuheshimu atakutumia. Atakutumia kuleta mapinduzi, atakutumia katika vita, atakutumia katika injili, atakutumia katika uamsho, atakutumia katika uimbaji hata katika biashara. Si wote wafanyao hayo hutumiwa na Mungu, ila wako ambao Mungu huwatuma na kuwatumia katika hayo.
Aliwatumia Yefta na Daudi katika vita, alimtumia Yeremia katika unabii, alimtumia Sauli katika ufalme na Musa na Haruni katika Ukuhani. Alimtumia Mariamu katika kumleta mkombozi Yesu na Elizabeth katika kumleta mwijilisti Yohana mbatizaji. Atakutumia pia.
Lakini Mungu ana kanuni moja, anamtaka mtu ajitenge na uovu. Kama unataka heshima mbele zake basi ni lazima ujitenge na ouvu. Ukikimbia dhambi atakuheshimu, ukishinda vishawishi atakuheshimu pia. Heshima si neema, ni jambo la kuamua. Heshima huleta na mafanikio, na mafanikio anayotaka Mungu kuyaona kwetu ni ushindi dhidi ya dhambi.
Katika nyumba kuna vyombo vyenye heshima na visivyo na heshima. Vya dhahabu hupata heshima kubwa kuliko vya udongo na vya mbao au miti. Ni wewe ndiye mwenye jukumu la kuchagua uwe chombo cha dhahabu, chombo cha udongo au cha miti. Njia ni moja kujitenga na uovu. Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina. Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema.” 2Timotheo 2:21
Mtu aliyejitakasa, anaheshima mbele za Mungu kuliko wapigania uhuru waovu, kuliko mastaa wazinzi, kuliko matajiri watoa kafara, naam kuliko watumishi wa Mungu wasiohubiri kweli ya Kristo ili kujipatia faida.
Tukijitenga na uovu Mungu atatuheshimu. Tutakua lulu kwake na dhahabu. Atatutumia sana kwa ngazi nyingine na kwa viwango vya juu. Kila siku nimekuwa nikimshukuru Mungu kwa kutupa upendeleo wa kuwa watangazaji wa injili. Ndiyo angeweza kuchagua wachina tu kwani wako zaidi ya bilioni moja, akikuchagua amekupendelea. Tafadhali jitakase.
“Oh! Choose to be a gold vessel”