Ndio maana haukuweza
Zingatia Uhalisia Gal 6:7
Imewatokea wengi
kushindwa kufikia malengo, ni jambo la kawaida kwa wengi kushindwa kupungua
uzito, si ajabu kwa wanafunzi kufeli mtihani. Kila unaposhindwa jitahidi kurudi
kwenye misingi. Wakristo wengi wameanguka katika dhambi na kwao ni muhimu
kurejea katika misingi.
Mambo hayatokei
yenyewe tu, na kama wakristo tunahitaji miujiza na si maajabu. We need miracles
not magic! Maajabu yako hata kwa waganga wa kienyeji, maajabu ni kupata pesa
bila kufanya kazi, kufaulu bila kusoma, kahaba kuolewa au asiyehaki kuinuliwa.
Ni ajabu kwa anayekula kupita kiasi kupungua uzito.
Miujiza ni tofauti na
maajabu. Miujiza inakutaka ushirikiane na Mungu, miujiza inatualika tuungane na
Mungu. Miujiza ni mchanganyiko wa sala na kazi, pia miujiza ni mchanganyiko wa
imani na matendo. Miujiza hutokea pale watu wanapoamua itokee. Amesema Joel
Osteen “Ni imani yetu ndiyo huamsha nguvu ya Mungu”.
Ili muujiza utokee
lazima pawepo na imani, sala, mafungo, bidii ya kazi upendo na amani. Upendo
unachagiza sana uwepo wa muujiza. Ofisi ambayo upendo umetawala watu watamaliza
kazi kwa wakati (finishing before deadline). Maajabu hutokea tu bila sababu,
lakini miujiza inahitaji muda, uwekezaji, bidii na upendo. Mungu wetu ni mtenda
miujiza (miracles) si maajabu (magic). Kama hauna muda na mpenzi wako usitarajie
muujiza wa amani na upendo bali tarajia maajabu ya amani na upendo. Galatia 6:7
Maajabu yanafanya
muuzaji mwenye lugha mbaya apate wateja, muujiza hutokea pale muuzaji mwenye
busara na kauli nzuri anapopata wateja wengi na kuuza sana sana. Waganga wa
kienyeji (chief magic promiser) hawakufundishi huduma nzuri kwa wateja bali
wanawahadaa wateja na kufanya upate usichostahili. Usiende kwao, wala kwa
wasoma nyota. Wagalatia 6:7
Hata biblia imekataa,
kuvuna usipopanda, kupewa usichoomba, kupata usichostahili. Wengi tunao ujuzi
wa kutufikisha kileleni, lakini hatuna maarifa ya kutufanya tudumu hapo. Haifai
kupenda kuona maajabu. Maajabu hayawezi kudumu maana hata hatujui kwa nini
hutokea. Lakini muujiza wa Yesu ukitokea na sisi tunajua tukitimiza
yanayotakiwa utatokea tena. Siku moja mpwa wangu alimuona Pastor Chris
akiwapuliza watu wanaanguka baadaye na yeye akafanya na akapata matokeo yale
yale. Siku za mbeleni nami pia katika kuombea watu nikafanya nikapata matokeo
yale yale.
Ushindi ni tabia,
mafanikio ni tabia pia. Soma biblia na tazama tabia za waliotendewa miujiza
utakuta zinafanana. Si rahisi kuushinda ulimwengu kama bado haujajishinda
mwenyewe, si rahisi kuaminiwa na watu ikiwa bado haujimini wewe mwenyewe.
Madhara ya kutokujiamini ni sawa sawa na kutokumwamini Mungu.
Batromayo kipofu
alihakikisha anapaza sauti na Yesu akamsikia licha ya kelele za umati mkubwa,
Zakayo alipanda juu ya mti ili amwone Yesu, mama aliyetokwa na damu alipenya
katika ya kundi la watu maana haikuwa rahisi kumgusa Yesu. Muujiza unataka
ujipange, uwe juu ya viwango vya watu, muujiza utataka upige kelele mpaka Yesu
asikie, muujiza unataka upenye katikati ya watu katika usaili.
Mara ya kwanza
ulipoimba vizuri Mungu alitaka ujue kipaji chako, pale ulipohubiri vizuri Mungu
alitaka ujue wito wako, pale ulipotengeneza bidhaa nzuri Mungu alitaka ujue
kazi yako lakini utambulisho huo haukusaidii kama hautendi hivyo mara kwa mara.
Kwa mshindi kushinda ni mazoea, kipaji chako kikiwa tabia yako hapo utadumu.
Wiki hii ikawe mwanzo
wa miujiza katika maisha yako katika jina la Yesu Kristo. Amen
0 comments :