Unatatua changamoto gani?
UNATATUA CHANGAMOTO GANI?
Ili kuishi
maisha yenye hamasa, swali muhimu unalotakiwa kujiuliza sio unataka kufanya
nini katika maisha yako ya kuwa hapa duniani bali unatakiwa kujiuliza ni changamoto
gani au tatizo gani unataka kulitatua katika kuishi kwako? Moja ya sifa kuu
ya kufanana kwa watu wote waliofanikiwa ni utatuzi wa changamoto; nioneshe
mtu aliyefanikiwa nikuoneshe changamoto anayotatua au aliyotatua katika kuishi
kwake. Katika ulimwengu huu, usitafute jambo la kufanya; tafuta
changamoto ya kutatua.
Kila
aliyezaliwa na mwanadamu amebeba jawabu la changamoto fulani; kwa sababu
mafanikio ya kweli yamebebwa katika kuleta majibu juu ya changamoto au upungufu
uliopo mahali fulani. Watu hawatakufuata wala kukulipa kwa sababu una kipawa au
ujuzi au uwezo fulani ndani yako, watu watakufuata na kuwa tayari kukulipa kwa
sababu kipawa chako, ujuzi wako na uwezo wako unatatua changamoto walionayo.
Thamani yako mbele ya watu inategemea kiwango chako cha utatuzi wa changamoto
walizonazo watu hao.
Boresha uwezo
wako wa kutatua changamoto.
Kila mara ni
muhimu kuboresha uwezo wako wa kutatua changamoto, ndio maana hata
watengenezaji wa simu kila mara huboresha simu wanazotengeneza kwa kuziongezea uwezo
wa kutatua changamoto mbali mbali. Ndio maana utasikia iPhone 5 mara iPhone 6
mara “iPhone 6 plus”. Wanachofanya hapa si kutengeneza simu nyingine bali ni
kuboresha simu iliyotengezwa hapo awali. Na kwa sababu hiyo thamani ya iPhone 6
plus ni kubwa kuliko thamani ya iPhone 6 ya kawaida. Na watu wako tayari kulipa
zaidi kwa iPhone 6 plus kuliko iPhone 6 ya kawaida kwa sababu “iPhone 6 plus”
imeboreshwa uwezo wake wa kutatua changamoto ya mawasiliano.
Kuna namna
nyingi za kuboresha uwezo wako wa kutatua changamoto katika eneo lako la
huduma, biashara, tekinolojia, uongozi, elimu ulipata, uandishi, ofisini,
kipawa, michezo (athletes); baadhi ni kwa kutafuta ujuzi zaidi, ‘kupractice’
zaidi, kujifunza kwa waliokutangulia, kujifunza kwa waliofanikiwa, kusoma
vitabu vinavyohusiana na eneo umalotaka kulifanyia kazi n.k. Wazo kuu hapa ni
kujitahidi kuwa bora zaidi ya jana, tafuta kuwa bora (excellent) katika kila
ulichoweka nia ya kukifanya.
There’s a place
for you at the top
0 comments :