Kwa mara ya mwisho
[USIPOZUIA LEO HUWEZI KUZUIA KESHO]
Inaweza ikawa ni ahadi ya uongo, kujiahidi
kupita uwezo wetu wa utendaji. Ngoja nile kwa mara ya mwisho, ngoja ninywe kwa
mara ya mwisho, ngoja niende kwa mara ya mwisho, ngoja nikakae naye kwa mara ya
mwisho. Tunaweza kushinda jaribu la kesho leo, kamwe huwezi kushinda jaribu la
kesho bila ya kushinda leo.
Inawezekana unajitahidi kupunguza ulaji wa
sukari, inawezekana unajitahidi kuacha kilema fulani au unahitaji kupunguza
kiasi cha unywaji wa soda. Unaweza tu kwa kuondoa urasimu wa mpaka kesho, mpaka
mwezi ujao au mpaka juma lijalo. Usianguke leo ili usimame kesho, badala yake
simama leo ili kesho usimama imara zaidi. Mwenye hekima mmoja anaandika: “Giving
in even once weakens our ability to resist next time”
Hujachelewa bado, wala haujaharibika
kabisa, you are not beyond repair! Usijikatie
tamaa mabadiliko yanawezekana. Siku 365 za mwaka ni fursa 365 za kubadilika.
Neema ipo kila asubuhi kwa hiyo unaweza kubadilika bila shaka.
Kuna nyakati huwa najiona niko chini (very
down) kwa sababu ya dhambi, makwazo, majaribu na pengine kiburi changu dhidi ya
neno la Mungu. Lakini huwa najitia moyo nikiwa na hakika kwamba, Mungu
hakuniumba ili anihukumu bali ili aniokoe na kunipa uzima wa milele katika YESU
KRISTO. Nikikumbuka neno hili huwa nafarijika sana, “Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate
wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo;” 1Wathesalonike5:9
Kuna mwingine anaweza akasema Mungu anajua
tutakwenda jehanamu, kwa hiyo hakuna haja ya kufanya jitihada. Wazo hilo si la
kweli, Mungu anajua utakwenda mbinguni kwa hiyo fanya jitihadi za
kumtafuta. 1Watheselonike 4:9
inaweka wazi kwamba Mungu hakutuumba kwa ajili ya hukumu.
Yesu aliposema, haombi kwa Baba atutoe
ulimwenguni bali atulinde na yule mwovu alimaanisha, Changamoto zipo, na hakuna
aliyekingiwa changamoto (no one is immune
to challenges) sote tunapaswa kupambana na kushinda. Unapotatua changamoto
moja unatengeneza kinga ya kukusaidia kupambana na changamoto nyingine, ndivyo
wasemavyo wenzetu kwamba; “bahari shwari haitoi wanamaji shupavu.”
Utapitia mengi katika bahari ya maisha; ila uwe na hakika Mungu anakuwazia mema
na mwisho wake utatoka katika bahari ya maisha ukiwa shupavu na hodari. Yako
mateso na ziko changamoto, yote hayo yapo ili kufanya uwe bora zaidi na uwe
shujaa zaidi.
Bila jangwa huwezi kuwa na Musa mpole na
mtaratibu, bila ubaguzi wa rangi huwezi kuwa na Nelson Mandela mwenye kusamehe
na mwenye heshima; bila ya kufeli au kuishia njiani ki-masomo tusingelipata
watu bora kama Bill Gates ambao laiti wangefaulu masomo yao vizuri na kuhitimu wangekuwa
waajiriwa wala wasingeliweza kujiajiri na kuajiri maelfu kama walivyo sasa.
Endelea mbele Yesu Kristo yu hai kwa ajili
yako. Shallom……
0 comments :