Sala ya mwaka mpya
(EE, BWANA UNIUMBIE MOYO SAFI)
Mipango
ya mwaka mpya 2017 bila badiliko la moyo na mtazamo ni kazi bure, ni sawa na
kufukuza upepo. Sasa ni mwanzo wa mwaka ambapo kila mtu ana mipango lukuki. Iko
ya kitabia, maana tungependa kuwa watakatifu Zaidi 2017, iko ya kiuchumi, maana
hutupendi umasikini, iko ya kijamii maana tungependa kuwa na Amani na watu wote
na kusaidia jamii zetu mwaka huu.
Katika
kuanza mwaka nilipenda kuwasikia watumishi wengi wa Mungu wanasema nini kuhusu
mwaka mpya 2017. Lakini katika wote na yote mimi nimeguswa na badiliko la moyo
ambalo amelisema Billy Graham ambaye ni mhubiri mashuhuri tena mwenye alama.
Kwamba, kama BWANA hakuniumbia moyo safi basi sitaonja badiliko lolote mwaka
huu. Lakini kama mioyo yetu na mitazamo yetu kama haikubadilika basi mipango
hiyo yote itakuwa ni bure. Ni lazima kufanywa upya nia zetu. [Warumi 12:1-2]
Moyo
wako ndio kitovu cha mabadiliko yote. Moyo hutoa badiliko la kudumu, na ili
badiliko liwe la kudumu lazima litoke katika msukumo wa ndani na si kutoka nje.
Mimi pia nina mipango mingi mwaka huu lakini huu ni kipaumbele, ninataka
badiliko la moyo, niwe safi zaidi na nifanane na Yesu. Ni muhimu tumwambia
BWANA abadilishe mioyo yetu. Oh Lord Jesus,
change my heart!
Unaweza
ukajipinga mwenyewe, ikiwa mtindo wako wa maisha hauna uhusiano chanya na
malengo yako basi tegemea 2017 kukuonesha mabadiliko kidogo sana. Ni vigumu
kukua kiuchumi bila kupunguza matumizi ya anasa, wako wanaotaka kubadilika bila
kumwomba Yesu abadilishe mioyo yao. Daudi alijua hawezi kujibadilisha wala
hawezi kubadilika ikiwa Mungu si chanzo na egemeo la mabadiliko hayo. Haya ni
maneno yake Daudi akihitaji badiliko kutoka dhambini mpaka katika utakatifu
tena, Ee, Mungu uniumbie moyo safi…” Zaburi 51:10
Katika
orodha ya mipango yako ya mwaka huu, ongeza mmoja, ongeza badiliko la moyo,
fanya jambo hilo kuwa mpango mkuu.
Kila
la kheri katika 2017.
0 comments :