Tunaishi mara moja tu!
(Tumia vizuri awamu yako ya maisha)
“tena alikufa kwa ajili ya wote,
ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili
yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao.” 2 Kor 5:14
Tungelikuwa
tunaishi mara mbili angalau mtu angeweza kutumia awamu ya kwanza kuishi kwa
ajili yake mwenyewe na awamu ya pili kuishi kwa ajili ya Yesu Kristo. Kizuri
zaidi ni kwamba, tunaishi mara moja, hakuna mtu mwenye awamu mbili za maisha. We live only once!
Katika
kuishi kwetu mara moja ni lazima mtu aamue kuishi kwa ajili yake mwenyewe au
kuishi kwa ajili ya Kristo. Wewe unaishi kwa ajili ya nani? Wako wanaoishi kwa
ajili ya kazi zao, wako wanaoishi kwa ajili ya michezo, wako wanaoishi kwa
ajili ya burudani na wako wenye hekima wachache wanaoishi kwa ajili ya Kristo.
Oswald
J Smith mwandishi wa kitabu nilicho kisoma na kukirudia zaidi ya mara mbili, “The Consuming Fire” anasema, “I have only one life to live and I want to
invest it for Thee” kwa tafsiri yangu, “Nina maisha haya tu, ninataka
niwekeze kwa ajili yako BWANA”
Katika
mstari unaotuongoza pale juu 2 Kor 5:14 Paulo Mtume anasema wazi Yesu anatutaka
tusiishi kwa ajili ya nafsi zetu wenyewe bali kwa ajili yake. Jiulize, unaishi
kwa ajili ya Kristo au kwa ajili yako mwenyewe?
Asubuhi
mpaka jioni unafanya nini? Wanaoishi kwa ajili ya Kristo huomba kwa saa moja na
kusoma neno kwa angalau saa moja. Pesa zako zinatumikaje? Wanaoishi kwa ajili
ya Kristo hutumia pesa zao kwa uinjilishaji. Luka 8:3
Nakualika
ujitoe kwa Yesu na kuishi kwa ajili yake kuanzia leo: Sema sala hii, “Ee BWANA
YESU mimi ni mwenye dhambi na wewe ni mwokozi wangu. Naomba unisaidie
kuanzia leo niyatoe maisha yangu kwako, wala nisiishi tena kwa ajili yangu na
kwa ajili ya Dunia badala yake nikufuate wewe milele. Amina.”
Nakutakia
msimu mwema wa sikukuu, Shalomu….
>
0 comments :