Kupatwa kwa jua
KUPATWA KWA JUA.
(Wafu hawawezi
kumchagua Yesu wala kumkataa shetani)
Alhamisi,
Septemba Mosi ilikuwa siku ya kupatwa kwa jua. Maeneo mengi ya mkoa wa Mbeya
hususani Rujewa yalishuhudia kufifia kwa mwanga na giza kutokea kwa masaa
kadhaa. Naamini ilikuwa hivyo kwa maeneo mengi ya Tanzania na Afrika Mashariki
kwa ujumla.
Kituo
cha habari cha BBC kilifanya mahojiano na Mheshimiwa Ghalib Bilal kuhusu
kupatwa kwa jua na hapo nikataka kusikia machache kuhusu jambo hilo. Katika
mahojiano hayo dondoo kubwa niliyopata ni kwamba, “kupatwa kamili hutokea mara
moja katika eneo fulani kila baada ya miaka 300.” Kupatwa kamili kwa jua
kutatokea tena hapa nchini kwetu miaka 360 ijayo. (At any place on Earth, a Total Solar Eclipse can be seen on average
once every 360 years.). Only my grave will witness that.
Miaka
mia tatu ijayo mimi wala wewe hatutakuwepo. Kumbe hatuna nafasi ya kuona tena
kupatwa kamili kwa jua tukiwa Tanzania. Tunachoweza kukiona tena ni kupatwa kwa
kawaida tu ambako hutokea mara kwa mara na si kupatwa kamili. Je, utakuwa wapi
miaka mia tatu ijayo? Je, ratiba yako ya siku inakupa kujiandaa na maisha hayo
ya umilele?
Ni
vema kujiandaa! Ni ukweli ulio wazi, dhambi ni kikwazo cha maandalizi yetu.
Kama ilivyokuwa kwa Adamu watu hawatendi dhambi kwa bahati mbaya au kwa
kudanganywa, bali hutenda kwa kuchagua. Yesu alikuwa kijana na alijaribiwa kama
sisi na hakutenda dhambi. Dhambi ni uchaguzi. Tunatenda kwa sababu tumeamua
kumkana na tumechagua kutenda. We sin not
because we have to, but it is because we want to.
Kila
siku watu zaidi ya mia moja hamsini hufariki, magaidi nao wanasababisha vifo
katika halaiki za watu. Kuuawa na gaidi hakukufanyi uokoke,
unamuhitaji Yesu kwa umilele wako. Mamia ya wanachuo wa Garisa huko Kenya
waliuawa na magaidi wa alshababu; tukio hilo haliwapi marehemu hao kumwona
Mungu ikiwa hawakumchagua Yesu wakati wa uhai wao.
Ukimkataa
Yesu ukiwa hai huwezi kumkubali ukiwa kaburini, ndio maana hakuna nchi duniani
ambayo marehemu wanapiga kura. Wafu hawawezi kumchagua Yesu wala kumkataa
shetani. Ni walio hai tu ndio wana uwezo huo. Dereva mmoja akielezea
uzoefu wake wa kesi za ajali za barabarani alisema, “Marehemu hashindi kesi.”
Ukikosa
kufika mbinguni huwezi kukosa kufika motoni. Wasio kwenda mbinguni huenda
motoni. Watu wengi hawavutiwi sana na kwenda mbinguni kwa sababu hakuna
walichowekeza huko. Hawajawekeza tumaini, imani, upendo, fedha wala matendo
mema; hakuna wanachotazamia kukiona wakifika huko, ndio maana hawana fikra za
kwenda huko.
Donald
Trump anapokwenda Uingereza anakwenda kuona alichowekeza, Dangote anapokuja
Tanzania (Mtwara) ni kutazama alichowekeza huko. Tukiweka pesa zetu mbinguni,
tukikataa mambo ya dunia basi bila shaka shauku yetu ya kwenda mbinguni
itaongezeka mara dufu maana tumewekeza huko. Hakuna mfanyabiashara anayeridhika
kwa kupata taarifa za simu tu bila ya kufika eneo ilipo biashara yake
ilikujiona kwa macho kinachoendelea, vivyo hivyo haitoshi kusikia tu simulizi
za mbinguni ni lazima siku moja tufike huko.
Yesu
alikuja kwa sababu ya walio wake, na sisi hatuna budi kumfuata aliko kwa sababu
Yesu ni wetu. Tukiwekeza hazina yetu mbinguni tutatamani kwenda kwa sababu
hazina ya mtu ilipo na moyo wake upo. Jifunze huduma kama hawa wa Luka 8:3
ambao waliamua kuhubiri na Yesu kwa fedha zao: “na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na
wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao.”
BWANA AKUBARIKI
0 comments :