Nataka kuwa kijana milele

6:19:00 PM Unknown 0 Comments

 
NATAKA KUWA KIJANA MILELE

“Forever…. Forever… I wanna be young”, “Milele… Milele… nataka kuwa kijana” Ni kibwagizo katika chaneli ya vijana wa Afrika Mashariki yaani East African Tv maarufu kama Chanel  Five. Kibwagizo hicho kinaonesha wazi namna vijana wanavyopenda ujana na hawako tayari kumaliza maswala ya ujana kwa haraka. Watu wengi wanatamani kurudi utotoni na wazee vijana wanaongezeka kila kukicha.
Msanii mmoja anasema, “ni binadamu peke yake ambaye hukaa na watoto wake kwa zaidi ya miaka kumi na nane.”  Viumbe wengine hawalei kwa kitambo kirefu, wanawajengea watoto wao uwezo wa kujitegemea mapema na kisha wanawatenga. Tai hakai na makinda yake kwa miaka kumi, hata wanyama wa kufugwa hawafanyi hivyo.
Vijana wengi leo si washirika wa maendeleo. Wamejikita katika burudani na michezo isiyo na tija. Wengi wanajaa katika mabanda ya video ili kutazama mechi na  kucheza michezo ya ku-beti. Kundi kubwa la vijana ni watazamaji wa maendeleo. Wanatumia kuliko kuzalisha, wanaisha bila tafakuri ya maisha. Tunahitaji kukua!
Wengi wanachangamkia yasiyofaa, wanajitahidi kufanya yasiyotakiwa. Vijana wamefanikiwa katika mambo yasiyo na tija. Maneno ya Francis Chan ni dhahiri:  “Our greatest fear should be of failure but of succeeding at things in life that don’t really matter”
 Vijana wengi waliofanikiwa wanasifa zifuatazo:
  1. Wametoa changamoto katika magumu yaliyo wakabili. Kila kijana anapaswa kuleta utatuzi dhidi ya dhahma inayomkabili. (Challenge your status quo-the mess your in) Ili kujipima mchango wako katika jamii kama kijana ni lazima uone namna ulivyopambana na mazingira mabaya yanayokukabili. Inaweza ikawa ni ombwe la umasikini, talaka, rushwa, uongo, mmomonyoko wa maadili na kadhalika
  2. Wanahoji. Wengi waliofanikiwa ni waliothubutu kuhoji kuhusu kuvuja vuja kwa imani ya dini yao, kuvuja vuja kwa maadili ya viongozi, kushuka kwa uchumi na hata kutaka kujua sababu zinazopelekea mambo fulani fulani katika jamii yawe kwa namna yalivyo.
  3. Waliofikiri kuhusu kesho. Vijana wanaofanikiwa ni wanaosumbukia hatima zao za baadaye kuliko mambo ya leo. Biblia inasema, “mwana mwenye hekima huweka akiba ya baadaye lakini mpumbafu hula vyote”
  4. Wanajali umilele wao. Ili kukaa na Mungu daima Mbinguni ni lazima kuhusiana naye daima hapa duniani. Kijana mwenye hekima anapaswa kujali mambo ya milele kuliko ya kisasa. What is eternal matters much than what is current!
  5. Wenye ujasiri. Umewahi kuwaza ni mambo mangapi ungetimiza kama usingeliogopa? Ili uende mbele lazima uanze leo. Ogopa kuogopa. Kijana ni mwenye nguvu, mwenye nguvu akiogopa hakuna atayethubutu. Mark Twain Yule mshairi maarufu aliandika: “The secret of getting ahead is getting started”
Mpaka wiki ijayo…Shallom!!1

0 comments :