Sitaki kukosa baraka hizi
Ilikuwa
mwezi Desemba 2015 nikiwa katika basi la Mbeya Express kuelekea Mpanda huko
Katavi. Kama ilivyoada nilikuwa na kitabu changu mkononi ili kurahisisha safari
yangu. Na katika mapumziko hayo mafupi ya siku kuu ya Chrismas niliamua
kuchochea uinjilishaji kwa kusoma kitabu hicho cha mwandishi Marc Cahil, “One
Thing You Cannot Do In Heaven”
Kitabu
kinahusu uinjilishaji tena si rahisi kukutana na ujumbe mwingine katika kitabu
hicho ambacho nilikuwa nakisoma kwa mara ya pili. Wakati huo hali yangu ya
uchumi ilikuwa si nzuri, ingawa nilikuwa nakwenda likizo nilikuwa nakwenda
nikiwa na wazo la kupunguza matumizi. Nilikuwa natembea nikiwa na tahadhari
kichwani, ya kupunguza matumizi hususani ya fungu la kumi. Ghafla ndani ya
kitabu nikakutana na onyo, “Unapotaka kupunguza matumizi usipunguze pesa ya
sadaka au fungu la kumi”
Yaani,
unaweza kupunguza matumizi ya nguo; chakula, vinywaji, safari na mengine lakini
si matumizi ya sadaka na zaka. Niliposoma ujumbe huo nikaweka azimio moyoni
kwamba sitapunguza matumizi ya zaka badala yake nitatoa kama ilivyokawaida 10%.
Ilinisumbua kidogo kwani nilikuwa nimepanga tayari kupunguza matumizi ya sadaka
ili kumudu mambo mengine.
Mwandishi
alinukuu maandiko kutoka katika Biblia jinsi Mungu atakavyo fungua madirisha ya
mbinguni na kunibariki hata isibaki nafasi, nilisoma pia namna atakavyo nilinda
na kuondoa hali ya kuvuja kiuchumi. Baada ya kuzisoma ahadi hizo niliandika
pembeni ya kitabu maneno haya, “siko tayari kukosa Baraka hizi” yaani, “I am
not ready to forfeit these blessings.”
Nilipofika
nyumbani niliamua kumtolea Mungu bila kupunguza kiwango licha ya changamoto
iliyokuwapo. Nilipomtolea Mungu alinibariki mno tena kwa haraka akinipa zaidi
ya mara tano ya sehemu niliyotoa zaka ndani ya siku saba. Kila ninapotoa fungu
la kumi ninamwona Mungu. Mara nyingine umeme uliachiliwa pasipo kupoozwa vema
na watu wengi walishuhudia uharibifu wa mali, jirani yangu pia alishuhudia vitu
vyake vikiungua. Asubuhi wakati ananipatia taarifa ya kilicho tokea ndipo
nilisikia ndani yangu Roho akinikumbusha lile neno kwamba, tukitoa zaka kamili
Mungu atamharibu yeye aharibuye. Nami nikajua wazi ni Mungu aliyeokoa vitu
vyangu kutoka katika uharibifu wa umeme. Asubuhi hiyo niltamani niwashuhudie
jirani zangu kwa nini Mungu amelinda vitu vyangu lakini sikupata kibali kwani
wangeweza kutafsiri kama majigambo ilhali ni shauku yangu kuona wengi wanakata
bima kutoka mbinguni kwa njia ya fungu la kumi.
Mtu
pekee ambaye anachukia kutoa fungu la kumi ni yule ambaye hawajawahi kutoa na
hivyo hajaonja baraka za kutoa zaka. Kwa sisi tulio onja kwa kweli, hatuwezi
acha tabia hiyo. Anthony Robbins anashauri watu kuweka akiba moja kwa moja
lakini mimi nashauri tutoe zaka moja kwa moja.
Hata
kama matumizi yako yameongozeka epuka kuacha kutoa fungu la kumi kwa sabau tu
eti matumizi yameongezeka. Toa hata katika hali ya shida. Tahadhari! Wengi
wametoa na huenda hawajaona Mungu akitenda kama nilivyoshuhudia. swali langu
kwao, walikwenda kutoa sehemu gani? Nimewahi kuulizwa, “Ni wapi nikatoe fungu
la kumi?”
Katoe
mahali unapolishwa kiroho, toa mahali wanapoliheshimu neno la Mungu, toa kwa
wale wanaotaabika kwa ajili ya kuwalisha watu chakula cha roho yaani neno.
Chunguza udongo na kisha toa kwa watumishi waadilifu. Mkulima anapaswa kuchagua
udongo, hali kadhalika tunapotoa zaka, sadaka na dhabihu lazima tuchague
udongo. Eneo unalopeleka zaka litakupatia neno kwa wingi, ukichunguza utaona
maeneo mengi ambayo watu hawatoi zaka hakuna neno. Mungu alisema tutoe zake ili
chakula (neno lake) liwe kwa wingi ghalani (Kanisani/fellowship/huduma na nk).
0 comments :