Chagua Heshima
Jitahidi uwe chombo
cha dhahabu
Watu
wengi wanapata heshima katika jamiii kwa sababu mbalimbali ambazo huhusisha pia
mafanikio yao. Lakini si wote wanaoheshimiwa na wanadamu huheshimiwa na Mungu
pia. Watu wengi tunapata heshima ya wanadamu huku tukikosa heshima mbele za
Mungu. Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya
udongo; vingine vina heshima, vingine havina. Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata
heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo
njema.” 2Timotheo 2:20-21
Mungu
akikuheshimu atakutumia. Atakutumia kuleta mapinduzi, atakutumia katika vita,
atakutumia katika injili, atakutumia katika uamsho, atakutumia katika uimbaji
hata katika biashara. Si wote wafanyao hayo hutumiwa na Mungu, ila wako ambao
Mungu huwatuma na kuwatumia katika hayo.
Aliwatumia
Yefta na Daudi katika vita, alimtumia Yeremia katika unabii, alimtumia Sauli
katika ufalme na Musa na Haruni katika Ukuhani. Alimtumia Mariamu katika
kumleta mkombozi Yesu na Elizabeth katika kumleta mwijilisti Yohana mbatizaji.
Atakutumia pia.
Lakini
Mungu ana kanuni moja, anamtaka mtu ajitenge na uovu. Kama unataka heshima
mbele zake basi ni lazima ujitenge na ouvu. Ukikimbia dhambi atakuheshimu,
ukishinda vishawishi atakuheshimu pia. Heshima si neema, ni jambo la kuamua.
Heshima huleta na mafanikio, na mafanikio anayotaka Mungu kuyaona kwetu ni
ushindi dhidi ya dhambi.
Katika
nyumba kuna vyombo vyenye heshima na visivyo na heshima. Vya dhahabu hupata
heshima kubwa kuliko vya udongo na vya mbao au miti. Ni wewe ndiye mwenye
jukumu la kuchagua uwe chombo cha dhahabu, chombo cha udongo au cha miti. Njia
ni moja kujitenga na uovu. Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya
udongo; vingine vina heshima, vingine havina. Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa
kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho
Bwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema.” 2Timotheo 2:21
Mtu
aliyejitakasa, anaheshima mbele za Mungu kuliko wapigania uhuru waovu, kuliko
mastaa wazinzi, kuliko matajiri watoa kafara, naam kuliko watumishi wa Mungu
wasiohubiri kweli ya Kristo ili kujipatia faida.
Tukijitenga
na uovu Mungu atatuheshimu. Tutakua lulu kwake na dhahabu. Atatutumia sana kwa
ngazi nyingine na kwa viwango vya juu. Kila siku nimekuwa nikimshukuru Mungu kwa
kutupa upendeleo wa kuwa watangazaji wa injili. Ndiyo angeweza kuchagua wachina
tu kwani wako zaidi ya bilioni moja, akikuchagua amekupendelea. Tafadhali
jitakase.
“Oh! Choose to be a gold vessel”