Ogopa Kougopa
(FEAR To FEAR)
Kuna
nyakati Mtunga zaburi amewahi kusema, “Ee nafsi yangu kwa nini kuinama (kufadhaika/kuogopa)”.
Ni wazi hakupendezwa na hofu, wala hali ya kutokujiamini iliyokuwa ndani yake.
Moja wapo ya sababu kubwa inayofanya watu wengi kushindwa kufikia kilele cha
mafanikio yao ni hofu ya kushindwa. Nashawishika kusema, hofu ya kushindwa
imewafanya watu wengi kushindwa kufikia mafanikio yao kuliko kushindwa kwenyewe
(Fear of failure has failed a lot of
people than failure itself)
“hofu ya kushindwaimewafanya watu wengi kushindwa kufikia mafanikio yao kuliko kushindwa kwenyewe”
Hata
watu wakuu walikutana na hofu walipoanza kutekeleza majukumu yao. Tofauti yao
na watu wengine, ni kwamba hawakuruhusu mashaka na hofu zao kuwa kubwa kuliko picha ya mafanikio iliyokuwa mbele yao (vision); na hivyo walisonga mbele na
kufanya mambo makubwa yaliyopata heshima katika vizazi vyao na vizazi
vilivyofuata baada yao. Walijua kuwa
picha ilikuwa ndani yao ni halisi kuliko mazingira ya hofu yaliyokuwa
yakiwazunguka kwa wakati huo.
Rick
Warren amewahi kuandika, “Kila tunaposhindwa, kuna uongo nyuma tuliouamini” (Behind every self-defeating act is a lie you
believe); hii ni kauli yenye kuhekimisha. Hofu ni moja ya uongo, hofu
hufanya watu washindwe masomo kabla ya mitihani, hupelekea bondia apigwe nje ya
ulingo, hofu huua kabla hata mtu hajafumba macho; hofu humpa mtu talaka kabla
ya ndoa.
Kuna
usemi usemao, “Njia ya muongo ni fupi.” Hofu ni uongo na hivyo njia yake ni
fupi. Tunaweza kuiaibisha hofu na kuikamata katika uongo wake kwa kuyafanya
yale yanayotutisha. Watu wakuu waliiaibisha na kuikamata hofu katika uongo wake
baada ya kwenda mbele na kufanya walioyaogopa kwa Msaada wa BWANA. Hofu
hutoweka tunapofanya tunayoyaogopa. Oh!
Mungu akusaidie kupata hisia za Daudi baada ya kumuua Goliathi. Oh Glory…I can feel it, how beautiful it
was, to kill what was scared by the whole Nation.
Kwa
sababu ya hofu ya kushindwa wapo waliokufa na biashara, makampuni, huduma,
sanaa, miradi na vumbuzi mbalimbali (zilizoishia kuwa mawazo na ndoto tu)
walizopewa kwa makusudi ya kuboresha maisha ya watu wengi katika vizazi vyao na
kwa ajili ya vizazi vitakavyofuata baada yao. Kila mtu ameumbwa kwa kusudi
maalumu, na kila mtu anacho kitu cha kuchangia katika kizazi chake na vizazi
baada yake; lakini kwa sababu ya hofu, vitu vingi vimebaki kuwa mawazo na ndoto
tu katika mioyo ya watu wengi.
Aliyeahidi ni mwaminifu.
Ili
kupata uhakika kama ahadi uliyopewa itatimizwa au haitatimizwa, jambo la
kuangalia si uzuri wa ahadi iliyotolewa bali mtu aliyetoa ahadi hiyo. Ahadi
inaweza kuwa nzuri lakini aliyetoa asiwe na uwezo wa kutekeleza. Ibrahimu
alijua siri hii muhimu; hata alipooneshwa picha, ya kuwa katika yeye mataifa
yote watabarikiwa, na mazingira yake hayakuonyesha kama jambo hilo litawezekana
jambo moja tu alijua nalo ni kwamba, Aliyeahidi ni mwaminifu hakika atatekeleza
alichoahidi. Ukweli huu ulinyima nafasi ya hofu kudhoofisha (paralyse) imani yake.
“Watu wakuu walishinda hofu zao kwa kuwa ndani yao walijua picha walionayo ndani ya mioyo yao ni halisi kuliko mazingira yao na tena imani yao haikuwa kwenye ahadi walizopewa bali imani zao waliziweka kwa Mtoa Ahadi”
Mungu
anapokupa wazo ulifanyie kazi au maono (vision),
mara nyingi mazingira yako hayatalingana na maono hayo. Hofu huwa kubwa pale
tunapoacha kuangali ahadi ya Mungu na picha iliyowekwa mbele yetu na kuanza
kuangalia mazingira au hali zinazotuzunguka kwa wakati huo. Watu wakuu
walishinda hofu zao kwa kuwa ndani yao walijua picha walionayo ndani ya mioyo
yao ni halisi kuliko mazingira yao na tena imani yao haikuwa kwenye ahadi
walizopewa bali imani zao waliziweka kwa Mtoa Ahadi.
“Lakini akiiona ahadi ya Mungu
hakusita kwa kutoamini, bali alitiwa nguvu katika imani,Akimtukuza Mungu. Huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza
kufanya yale aliyoahidi” Warumi 4:20-21 (msisitizo umeongezwa)
Vita
kubwa ya adui ni kutushawishi tusiamini na tutilie mashaka (doubt) juu ya kile ambacho Mungu amesema
katika Neno lake kuhusu maisha yetu; kuamini kuwa unao uwezo ambao Mungu
amesema unao; ya kuwa unaweza kufanya mambo ambayo Mungu amesema unaweza
kufanya; unaweza kupata mambo ambayo Mungu amesema utapata amba kuwa Mungu
anaweza kufanya yale aliyoahidi.
Kukosekana
kwa imani huipa hofu nafasi ya kukua, kuongezeka kwa mizizi yake ndani yetu,
hata kuwa mikubwa kiasi cha kutuzuia kufikia matarajio na mipango yetu ya kila
siku; Pale tunapoanza kuamini uongo tu; ndipo uongo huo huanza kuwa dhahiri
(manifested) katika maisha yetu (Ayubu3:25-26). Muamini Mungu, kuwa anaweza
kutekeleza kile alichosema, na hakika atatekeleza kwa maana Yeye ni Kweli hakuna
uongo katika maneno yake! Mtu mmoja amewahi kusema, “Usitie shaka kumuamini Mungu anayejulikana; kwa ajili ya mambo
yasiyojulikana”
Tujifunze kwa Joshua na Kalebu.
Kuujua
ukweli huu utakupa fursa ya kuishi maisha yenye ujasiri utakao itupa mbali hofu
yako. Neno la Mungu na maono (vision) uliyonayo yanakupa uhakika na ujasiri
kwamba, haijalishi mazingira uliyopo sasa, jambo hilo au mazingira hayo ni kwa
muda tu kwa kuwa Aliyeahidi hakika atatimiza alichoahidi. Kama mazingira
uliyopo hayafanani na picha ya mafanikio iliyopo ndani yako, usitie shaka upo
hapo kwa muda tu.
Kama
ndani yako unaona picha (vision) unamiliki kampuni yako mwenye yenye lengo la
kuboresha maisha ya wengi na kumletea Mungu utukufu, basi mazingira yako ya
sasa kwamba umeajiriwa au huna hata ajira yasikutie hofu ya kutokufikia picha
hiyo. Kile usichokuwa nacho leo utakuwa nacho kesho, endapo tu utasonga mbele
kuelekea picha hiyo bila ya kusikiliza kelele zinazopigwa na hofu.
“Wakati wewe unaogopa kufanya upendalo ili kutimiza ndoto zako, wenzako wanaogopa kuogopa na hivyo wanafanya”
Wewe
pia ukimhesabu Mungu kuwa mwaminifu utashinda, hauna sababu ya kuogopa, kama
iko sababu ambai ya kuogopa hofu yako (to
fear your fear). Wakati wewe unaogopa kufanya upendalo ili kutimiza ndoto
zako, wenzako wanaogopa kuogopa na hivyo wanafanya. Sababu moja wapo inayofanya
tumwite Mungu katika sala ni ili kuondoa hofu zetu, tunapoomba tunakuwa jasiri
kama amba na hapo tunafanya hata kupita tuwazavyo. Daudi anasema, “Nalimtafuta BWANA akanijibu, Akaniponya na
hofu zangu zote” Zaburi 34:4!
Hiki
ndicho kilichowapa nguvu Joshua na Kalebu, waiijua ahadi ya Mungu; ndani yao
walikuwa na picha ya nchi mpya baada ya kuishi katika utumwa kwa muda mrefu.
Neno la Mungu na picha ya maono waliyokuwa nayo, iliwapa ujasiri wa kusonga
mbele hata pale walipokuta na mazingira ya kuwatia hofu. Kila walipokutana na
changamoto katika kufikia kilele cha mafanikio yao jambo moja walizingatia,
nalo ni kwamba, aliyeahidi ni Mwaminifu
na Hakika Atatimiza Alichoahidi. (Hesabu 13:30-31, 14:24)
See
you at the top…!
0 comments :