Kama si Kompyuta Basi ni Roboti
KAMA SI KOMPYUTA
BASI NI ROBOTI
(Tumia akili yako kufikiri vema)
Dunia iko kwenye kasi kubwa ya mabadiliko
ya sayansi na teknolojia. Mabadiliko haya ni muhimu sana, nchi ambazo ziko
mbele katika mabadiliko haya watu wake huishi maisha marefu. Si ajabu kwa
Japan, Korea kusini na Kaskazini raia wake kuwa na wastani wa umri mrefu wa
kuishi. Mabadiliko haya humpa mwanadamu muda wa kupumzika kwa kuwa humwondoa
kwenye majukumu ya kutumia nguvu na kumwachia jukumu zito la kufikiri. Sayansi
na teknolojia ni muhimu katika afya ya binadamu, usindikaji na ujenzi wa
miundombinu.
Kazi kubwa ambayo mwanadamu anapaswa kubaki
nayo ni kufikiri. Mabadiliko na mapinduzi hayawezi kutokea ikiwa hatukupindua
sehemu iliyoko katikati ya sikio la kulia na sikio la kushoto yaani, ubongo.
Kazi za mazoea kama vile kubeba mizigo, kubaki mizigo, kuandika hati,
kusikiliza na nyinginezo zifananazo na hizi zinaweza kufanywa vizuri kama sina
kompyuta basi ni roboti.
Hivi karibuni Japan wamezindua roboti
ambaye huangalia watoto nyakati za usiku. Bila shaka roboti huyu akifika Afrika
atanyang’anya kazi za watu wengi katika shule na maeneo ya malezi ya watoto.
Kupitia masomo ya walimu wabobezi yaliyoko mitandaoni, “you tube” na katika
maeneo mengine ya kuhifadhia itafika mahali hatutahitaji tena kukutana na
mwalimu ana kwa ana. Mungu alitaka tuishi kwa kufikiri, tutumie utashi wetu.
Kufikiri hakupitwi na wakati, mwenye fikra njema anaweza kushinda kipimo cha
muda (time test).
Tabia za mazoea na kazi za mazoea ni rahisi
kufanya kwa kutumia teknolojia pasipo kumhitaji mtu awaye yote. Tabia hizi za
mazoea huua ubunifu na uwezo wetu wa kufikiri. Wastaafu wengi wanaotoka kwenye
kazi zisizosumbua ubongo hushindwa kumudu maisha mapya ambayo huhitaji fikra
mpya na mawazo mkakati. Fedha yao ya kustaafu huwa kama magurudumu mapya katika
injini iliyoharibika kabisa. Ni wazi Teknolojia inawafukuza watu wengi kazini
kuliko tumbua tumbua ya vyeti feki. Uzuri wake ni kwamba inarahisisha utendaji
na ina ajiri watu wengi zaidi wanaoifahamu zaidi ya wale inaowafukuza.
Ni muhimu tuusukume ubongo na ufahamu wetu
ili tupate mawazo na fikra endelevu za kutuwezesha kwenda sambamba na sayansi
na teknolojia. Ni muhimu kukumbatia teknohama kuliko shahada za vyuo vikuu.
Nchi za wenzetu zinapunguza udahiri vyuo na zinahimiza ufundi ili tu zikuze
ujuzi na matumizi ya sayansi na teknolojia katika maisha ya kila siku.
Ile kwamba, mtakula kwa jasho haikuzuii
kufunga kiyoyozi na kula kwa damu ya Yesu iliyovunja laana zote. Jasho ni
matokeo ya ugumu wa kazi ni muhimu fikra zetu zituletee njia rahisi, zenye
kugharimu muda mchache, rasilimali chache na ubora wa juu. Tukutane katika
msimu mpya wa Weekend of Purpose. Barikiwa!!
0 comments :