UNATAKA KUFANIKIWA KATIKA NINI?- IV
UNATAKA KUFANIKIWA KATIKA NINI?-IV
(Amua kuthubutu)
Mtu mmoja amewahi kusema, “Maisha hayatupi
tunachokitaka, bali hutupa kile ambacho tupo tayari kukifanyia kazi”. Kile
ambacho unatamani kitokee katika maisha yako au katika eneo lolote la maisha
yako ni lazima uwe tayari kufanyia kazi ili kiwe halisi. Nioneshe mtu mwenye
udhubutu katika yale anayoyatamani, nikuoneshe mtu mwenye matokeo katika maisha
yake.
Kuhamasika (motivated) pekee katika jambo fulani hakutaleta matokeo katika
maisha kama hakuna udhubutu wa kufanyia kazi jambo hilo. Wako wengi waliopita
semina au kusikia mafanikio ya watu wengine, na wakahamasika kweli kufikia
malengo waliyojiwekea lakini baada ya muda hakuna wanachoweza kuonesha kama
matokeo ya kuhamasika kwao. Na hii ni kwa sababu walihamasika lakini
hawakuchukua hatua ya kufanyia kazi matamanio yao.
Mwenyehekima mmoja amewahi kusema, baada ya
mwaka kupita au mwezi au muda fulani, tutabaki tukijilaumu na kutamani kama
tungedhubutu kuyafanya yale tuliyoyahairisha. Do it today or regret tomorrow. Kumbuka: hakuna jambo lolote lenye
thamani ambalo huja kirahisi, ni matokeo ya kazi (nothing worth comes easy, it
takes work).
“Mtu
mvivu husema,Simba yuko nje; nitauawa katika njia kuu” Mithali 22: 13
Adui mkubwa katika eneo la udhubutu ni
visingizio; unaweza kuwa katika kundi la watu wanaoeleza kwa nini hawakuweza
kufikia malengo yao, au ukawa katika kundi la wachache wanaoleza namna gani
wameweza kufikia mafanikio yao katikati ya changamoto nyingi. Kumbuka,
ulimwengu hautoi heshima kwa wanaoeleza kwanini haiwezekani, au kwanini
hawakuweza au wanaoeleza namna ambavyo watu waliwakatisha tama walipotaka
kuanza. Usijipe majibu ya kushindwa au
kwamba haiwezekani kabla haujadhubutu. “Maisha hayatupi tunachokitaka, bali
hutupa kile ambacho tupo tayari kukifanyia kazi”.
There’s a
place for you at the top
0 comments :