Changamoto kwa viongozi vijana
(Usimzuie mtu
kufanya mabaya, ana uhuru)
Changamoto kubwa inayowasonga viongozi
vijana ni kumilikiwa. Kuna hatari ya viongozi vijana kumilikiwa au kuongoza kwa
akili za walioko nje ya ulingo. Kuna umuhimu wa viongozi vijana kuonesha
umakini mkubwa na kipekee.
Ili kummiliki kiongozi kijana watu hutumia
vitisho nini kitampata au nini hakitampata. Mara nyingi wenye roho hii (spirit of manipulation) husema, fanya
hivi ili upendwe na watu au usifanye hivi watu watachukia. Watu wenye roho hii
hutoa hakikisho feki, humwakikishia mtu usalama ambao kimsingi ni Mungu peke
yake atupaye kukaa salama katika kazi, biashara na vyeo. “Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana
Wewe, Bwana, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama.” Zaburi 4:8
Yesu alijua Petro anaroho hii ambayo hutoka
kwa shetani. Petro alimwita Yesu Kristo pembeni akimwonya kwamba, mateso
hayatampata. Mara nyingi wenye roho hii hupenda kumbana mtu pembeni, humwita
kipekee bila ya watu, hutoa onyo hilo kwa siri.
Ingawa Yesu Kristo alikuwa kiongozi kijana
hakusita kumkemea Petro kwamba, “rudi nyuma yangu shetani”. Nakusihi kijana
usiruhusu kumilikiwa kinyume na kusudi la kuumbwa kwako, usizuiwe kutekeleza
yale ambayo Mungu amekuitia kutekeleza. Mathayo 16:23
Nakumbuka nikiwa kiongozi kijana mtu mmoja
aliniita akinikemea na kunieleza fanya hivi au vile, na mara moja nikawa mkali
nikamwambia, “Mimi ni mtu wa kanuni, sipangiwi nifanye lipi na lipi nisifanye
bali napanga mwenyewe.”
Yes, I am
a man of Principle! Nilijibu hivyo waziwazi kwa sababu nilijua ubaya wa roho
hii ya kumiliki watu, nilikuwa nimeitafakari usiku wa kabla ya tukio. Mtu
anaruhusa ya kuchagua hata mabaya, uhuru wa kuchagua (freedom of choice) ni
muhimu kwa kila jamii ya kistaarabu. “Because
to take away a man’s freedom of choice, even his freedom to make the wrong
choice, is to manipulate him as though he were a puppet and not a person”
Madeleine L’Engle
Imani hufanya watu wamilikiwe lakini
maarifa huwaweka huru. Hakuna anayeruhusiwa kumiliki utashi na dhamira ya
mwanadamu. Hata viongozi wa dini hawaruhusiwi. Mwanadamu ni kiumbe huru, na
anapaswa kuamua apendacho.
Endelea kutembea katika uhuru wako, Mungu
alimtuma mwenaye kukuokoa na shetani ili uwe huru wala si ili uwe milki ya
viongozi wa dini, siasa au serikali.
Kumiliki watu ndio uchawi wa kisasa ambapo mtu hafanyi kitu bila ya
kupiga simu au kuomba kibali kwa wanadamu.
Amesema Joyce Meyer, Ukiwa na shida nenda
kwenye kiti cha enzi cha Mungu, usikimbilie kupiga simu. (Go to throne not to the telephone) Mtegemee Mungu na yeye atakuwa
ngome yako, ngao yako, na kigao wala hautaondoshwa.
Barikiwa.
0 comments :