Kipaji chako ni hiki hapa
KIPAJI CHAKO NI HIKI HAPA
(Katika taabu ni rahisi kujua kipaji chako halisi)
Nani ni nani Tanzania, Kuna watu
wanafuatana na utambulisho wao, Mchango wao na karama zao zimewatambulisha. Who is who in Tanzania? Sheikh Shaaban
Robert amejulikana kwa mashairi, Askofu Moses Kulola amejulikana kwa injili,
Rose Mhando amejulikana kwa nyimbo za injili. Wewe unautambulisho gani?
What is
your Identity? Tunaposhindwa kujua utambulisho wetu kupitia karama na
makusudi ya kuumbwa kwetu tunapoteza maana ya kuishi. Na hapa siku tukiimba
vizuri tutafikiri sisi ni waimbaji na siku tukifundisha vizuri tutafikiri sisi
ni walimu. Tatizo hili limewasumbua wengi na limekuwa likijulikana kama, The Crisis of Identity, ni hali ya
kutokujua utambulisho wetu na mchango wetu kwa jamii.
Ukitaka kukosa mshindi katika mchezo wa
mpira wa miguu usimpige refa bali ondoa magoli na hivyo kutakuwa hakuna sehemu
ya kufunga na tayari mpira utapoteza ladha. Kingine unachoweza kufanya ni
kuweka nguzo nyingi za magoli (yaani badala ya mbili weka nne). Malengo mengi
maishani ni usumbufu. Kuwa na malengo mengi hakukupi nafasi ya kuwa mshindi
ndio maana kila timu hufunga katika goli moja tu. Maisha bila ya kuwa na lengo kuu
la kufanikisha hayana ladha. Ndio maana ni muhimu kujua kusudi lako na kipaji
chako.
Kipaji halisi hujidhihirisha wakati wa
taabu, wakati ambao uko peke yako bila ya ulio wazoea. Unachopenda kufanya
gizani bila ya kuhimizwa na mtu kinaweza kuwa kipaji chako nuruni. Kipaji cha
ubondia hugunduliwa nje ya ulingo na ulingoni ni sehemu ya udhihirisho tu.
Yusufu alitabiri Gerezani, Paulo na Sila
waliimba na kumsifu Bwana wakiwa gerezani mpaka milango ya Gereza ikafunguka.
Je! kipaji chako kinadhihirika wakati wa shida? Kipaji halisi hakinyamazishwi
na mazingira magumu.
Kipaji au karama ya Mungu huonekana hata
katika taabu, Yesu aliendelea kuhubiri, kuponya na kuokoa hata akiwa msalabani.
Don’t be silenced by problems
Nimeona Mungu akiponya kwa uponyaji mkuu
katika mazingira ambayo sikuwa hata na utayari. Siku chache zilizopita tumeshuhudia
Boss mkubwa aliyeachishwa kazi TANESCO akiendelea na kuhubiri injili. Kawaida
ya kipaji halisi ni nyenzo inayotumika hata katika taabu, kamwe hainyamazi.
Umri haunyamazishi kipaji chako, ana miaka 82 ya kuzaliwa bado Jimmy Swaggart
anaimba, kupiga kinanda vizuri na kufundisha.
Wako wakimbizi waliotumia vipaji vyao
ugenini, wako watumwa waliotawala utumwani. Wako wafanyakazi wa ndani
walioishia kuwa wafalme. Ni baada ya kugundua vipaji vyao na kuvitumia hata
katika mazingira magumu. Endelea kutumia kipaji chako usikate tamaa.
Mazingira magumu yanapaswa kukuhamasisha
kutumia kipaji chako na si kukitelekeza kipaji chako. Kwa tafsiri yangu Paulo
alimaanisha hivi, “…chochea kipaji ulichopewa na Mungu kilicho ndani yako.” 2 Tim1:6
Kileleni ndipo
tunapopatikana
0 comments :