Weekend of purpose ya kesho
(Ni Jumamosi ya kesho 13/05/2017 kuanzia
saa tatu asubuhi)
Ni zaidi ya miaka miwili sasa tangu Mungu atupe wazo la kufanya , “Weekend Of Purpose” wazo
hili tulilipata kwa BWANA. Nyakati hizo baada ya kumaliza Chuo kikuu tulikuwa
tunakutana Tegeta siku za weekend kwa ajili ya kubadilishana mawazo, kusali, na
kutiana moyo katika harakati za muda huo na baadaye. Siku moja katika kuomba
kwetu ndipo BWANA alipotusemesha kuhusu jambo hili nasi tukalitenda.
Tukaanza
kuandaa “Weekend Of Purpose” ya msimu wa kwanza na hatimaye kesho itakuwa ya
tano. Ni siku mbili ambazo Bwana Alituambia tuwafundishe watu makusudi ya kuumbwa
kwao, kwamba anawajua na amewaumba kwa kusudi maalumu. Kazi yetu ni kukufanya
ujue kusudi la kuumbwa kwako na kukukumbusha umuhimu wa kulitenda na kukupa
mbinu za kulifanikisha pia. Yeremia 1:5
Siku ya mwisho,
wako watakaojuta kwa nini hawakufanya hili na lile, na wako watakaofuraha na
kusema, I am so glad I did! Raha ya
kifo cha mtu wa Mungu ni kutimiza kusudi. Kifo cha mtu wa Mungu kinamfurahisha
Mungu maana ni usingizi wa amani baada ya kazi. Ni faida kuu, kuishi kusudi
uliloitiwa na BWANA. Kifo ni kitamu kazi yako ikiisha vizuri, kinyume na hapo
ni janga. Zaburi 116:15
Tunazo shuhuda
za waliohudhuria Weekend Of Purpose ya kwanza na baada ya kujua kusudi la
kuumbwa kwao, waliacha yale yasiyo ya kwao na leo hii wanafuraha kwa sababu
wanatumikia kile ambacho Mungu alitaka wafanye.
Jaribu kufikiri
kama Petro angeendelea kuvua samaki milele, angetoa hesabu gani mbele za Mungu;
ambaye kwa hakika hakumweka awe mvuvi wa samaki, bali awe mhubiri wa injili.
Utajisikiaje siku hiyo Yesu akikwambia nilikuumba uwe nahodha wa meli ilhali
wewe umeishi maisha yako yote kama daktari wa meno. Ni kazi yetu katika Weekend
Of Purpose kukusaidia kujua karama na makusudi ya kuumbwa kwako. Mafundisho
yatakusaidia umalize vizuri sana, Zaburi 116:15
Katika “Weekend
Of Purpose” utajengwa kitabia kama mwenye hekima mmoja alivyosema, “iweni
watakatifu kwanza ndipo muwe wamisionari” neno hili ni kwa kila kada, iweni
watakatifu kwanza ndipo muwe madereva, iweni watakatifu kwanza ndipo muwe
wahandisi, iweni watakatifu kwanza ndipo muwe wagavi. Utajengwa ili tabia yako
ifanane na kazi yako na kusudi uliloitiwa. Mhasibu ukionekane katika taswira ya
fundi makenika (fundi wa magari) akiwa gereji bila shaka utaambiwa rudi
nyumbani kavae ki-hasibu. Tabia ni matendo na mazoea yanayohusu matamshi,
mavazi, matendo na mwenendo wote.
Karibu sana
kesho Jumamosi saa tatu, ukifika Mawasiliano au Makumbusho panda magari
yaliyoandikwa Bunju/Tegeta au Bagamoyo shuka kituo kinaitwa CHAMA KWA MASISTA-
pale BOKO, vuka barabara, elekea upande huo wa kuume wa kanisani mpaka
utakapoona geti la Masista wa Karmeli ambalo liko mbele baada ya kumaliza uzio
wa kanisa utakuwa umefika.
Hautajutia
kufika ni faida tupu, tukutane hapo. Mungu akubariki.
0 comments :