USIMDHARAU MSHINDANI WAKO.
(Don’t underestimate your rival)
Ikiwa mhitimu
wa chuo kikuu ataambiwa ajiandae kwa mtihahi wa darasa la kwanza, nadhani
maandalizi pekee atakayofanya ni kwenda kwenye huo mtihani ambao unaonekana ni
wa chini sana ukilinganisha na kiwango chake cha elimu. Lakini ikiwa ataambiwa
atafanya mtihani au unaofanana na elimu yake au zaidi bila shaka atajiandaa
sana.
Mshindani wako
au adui si lazima awe mtu inaweza ikawa ni hali fulani (situation/condition). Inaweza ikawa ni hali ya umasikini, hali ya
ugonjwa, kutokukubalika au vinginevyo. Mshindani wako inawezekana ikawa ni
tofauti ya mahali ulipo na pale unapotaka kwenda. Yote kwa yote ni lazima
tujizatiti, taking this battle very
serious!
Ukijua kwamba
mpinzani wako ni mwepesi (si lazima awe mtu) unaweza kufanya maandalizi mepesi
na ndio chanzo cha kuangamia kwako. Unadhani nini kinatokea kwa wanaojua
kwamba, kesho watashindana na mwanadamu mwenye kasi zaidi yaani Usain Bolt? Si
siri watajiandaa sana, wanajua mpambano ni wa kufa na kupona.
Nini kinatokea
kwa mzungumzaji anapojua katika mjadala huo atakuwapo Rais mstaafu wa Marekani
Barrack Obama pamoja na Baba Mtakatifu Papa Francis. Ni wazi mzungumzaji
atajipanga vilivyo, nini aseme na nini asiseme. Ukijua utazungumza mbele ya TD
Jakes lazima ujipange. Ukijua kwamba kesho utapambana na Mike Tyson (wakati wa
zama zake) na hujajiandaa vizuri, naamini utaomba udhuru kuliko kuweka maisha
yako rehani. Preparation is a key!
Maisha nayo
yako hivyo tunapaswa kuyaendea kwa kujiandaa kufa na kupona. Ukiwa shuleni
soma, kazini fanya kazi kwa bidii, katika biashara pia ni vizuri kuwa na weledi
wa kutosha. Ukiyadharau maisha ukisema ndege wa angani wanakula, tutakusubiri
tukuone na wewe kama utaruka kwa mbawa. Tutasubiri tuone kama na wewe utaingia
kwenye mashamba ya watu bila kibali kama ndege.
Kufurahia
maisha haina maana kutokujizatiti kufanya vizuri na kuishi hadhi ya juu. Si
kila mwenye nguo yenye kiraka ni bahati mbaya, wengine wanapata malipo ya kazi
yao. Wakati wenzao wanasoma wao walilala, wakati wenzao wananunua mashamba wao
waliongeza mke wa pili, wakati wenzao wanakwenda mazoezini wao walikwenda
kulewa pombe.
Usiyachukulie
maisha haya kirahisi, chukua wajibu wa kuyapanga na kupangilia. Wapenda hadithi
mnakumbuka hii, Sungura alipomtazama kobe alimchukulia kirahisi sana. Sungura
alimdharau kobe akiona hawezi kushindana naye katika riadha, hii ilipelekea
sungura kucheka sana kwa nini apambane na kobe. Mbio zilipoanza sungura
alikimbia kwa kasi na alivyogeuka nyumba aliona kobe yuko pale pale, Sungura
kwa dharau akaamua kulala. Hatimaye usingizi wa pono ukamkuta sungura, na
hatimaye kobe akampita na kutwaa ushindi. Japo kobe alikuwa taratibu alikuwa
akimaanisha kushindana na alikuwa amejizatiti kweli kweli. Somo, usiwe kama sungura,
take this life very serious!
Tukutane Boko
Karmeli kwa weekend of purpose timu nzima ya Life Minus Regret itakuwa pale
kuinjilisha na kufundisha na kusisimua. Usikose siku hiyo moja tu, itabadili kabisa maisha yako.
0 comments :