Unatakiwa Kwenda
UNATAKIWA KWENDA
Toka ulipo, piga hatua
Mathayo 7:7,
Ombeni na dumuni katika maombi, tafuteni mpaka mpate, bisheni na kuendelea
kubisha hodi mpaka mfunguliwe. Maneno yote haya yanaonesha umuhimu wa kupiga
hatua ili kupata (It’s about a constant
movement to achieve), hatutafuti katika eneo moja bali tunatafuta popote
mpaka tupate. Wachache tu ndio walioitwa wafanikiwe mahali walipo, wengi
wameitwa ili waende mahali fulani. Kuna mafanikio makubwa kwa wale watakao amua
kwenda. Mwaka huu ni wako, unaitwa kwenda shule, kwenda mji fulani, kujiunga na
chuo fulani, kwenda katika kikundi fulani au nchi fulani.
Katika kwenda
kwako utafanikiwa. Umeitwa kwenda kwa watoto, kwenda kwa masikini, wagonjwa na
wanafunzi. Kila mtu ameitwa kwa ajili ya watu fulani, wanaharati wameitwa kwa
ajili ya haki na uhuru wa raia na wanafanya hivyo kwa nguvu zao zote. Wako
walioitwa katika biashara, uongozi, uchungaji, uimbaji na uinjilisti, na
wanapaswa kwenda. Nenda ukaanze mwaka huu.
Musa aliwaendea
wana wa Israel hawakuwapo alipo yeye, Yesu alitujia ulimwenguni akitokea mbinguni,
Wakoma waliliendea jeshi la washami na mama Theresa aliwafuata masikini wa
Calcutta nchini India. Inakupasa kuwaendea, usisubiri wakufuate. It’s all about going!
Reinhard Bonnke
alitoka Ujerumani akaja Africa, Hudson Taylor alitoka kwao akaenda China kama
Mmisionari akiacha hata mchumba wake aliyesusa kuondoka. Ibrahimu alitoka kwa
Tera babaye akaenda mahali alipoitiwa na Mungu. You have to move!
Mamia ya watu
wanaothubutu kuondoka na kuanza jambo hufanikiwa, na hii ndiyo roho waliyonayo
waasisi wa mataifa na makampuni. Kuliko kufia kitandani kwako ni afadhali kufia
barabarani katika njia yako kulekea mafanikio yako.
Ni muda wa
kusimama, ni muda wako wa kutoka nyuma na kusogea mbele. Kuna nyakati moja
nilikuwa safarini nikitafakari huku nikiwa nimechoka na hali ya masiha yangu (status of life) na niliwaza kama ndoto
zangu zitatimia au hazitatimia na zimekufa. Naye Mungu akanijibu kwa wimbo,
“mwota ndoto hafi mpaka zimetimia”. Ndivyo ilivyokuwa kwa mwota ndoto Yusufu,
kwa mwota ndoto Barack Obama, kwa mwota ndoto Nelson Mandela na ndivyo ilivyo
kwako ikiwa unandoto za kufanya jambo fulani zuri la kushangaza dunia.
Usiishi bila
dunia yako, jiunganishe na kujiambatanisha na watu, watu ni kila kitu kwa mwota
ndoto. Haruni ni muhimu kwa Musa, wenye dhambi ndio wateja wa duka la Yesu,
masikini ndio wateja wa wanasiasa, wagonjwa ndio wateja wa madaktari. Tambua ulimwengu
wako, uendee, jiambatanishe nao.
Ukubwa ni namna
unavyotumikia kundi uliloitiwa na Mungu, na jinsi mwalimu anavyowatendea
wanafunzi wake. Tukutane mwezi wa tano, usikose Weekend of Purpose, msimu huu
wa tano BWANA amekuandalia mambo motomoto kuhakikisha unafanikiwa na ndoto zako
zinatimia.
Barikiwa……
0 comments :