Tumia akili zako ....
Zitumie, usizitumaini.
Akili zako
zitaimarika kwa sababu ya kutumika wala hazitachakaa. Akili huchakaa kwa
kutokutumika wala si kwa kutumika. Tofauti na akili, Vitu vingi huchakaa pale
vinapotumika sana (subjected to wear and
tear), vifaa vingi hupungua uwezo wake wa kazi na ufanisi kwa sababu ya
kutumika. Vingine hupungua hata thamani. Akili huimarika kwa kutumiwa na mwenye
nazo. Usizihurumie akili zako, watoto wadogo wanauwezo wa kujua lugha zaidi ya
saba na wala akili zao hazichakai. Wanaweza kuongea; kijerumani, Kiswahili, kifaransa,
Kiingereza, kihispania; Kichina, Kitaliano na kireno. Unaweza ukaona jinsi
akili yako ilivyolala kwa kushika na kutenda mambo machache.
Siri ya
mafanikio iko katika moyo wa kila kitu. Ni wajibu wetu kujua undani wa kila
jambo na kutafuta usahihi wake kabla ya kuliendea. Kufeli kunaanza kwa kufanya
usichokijua au kuungana na usiyemjua vizuri, au kwenda njia moja na usiyemjua
au ofisi ambayo maono yake hayajulikani. Know
the heart of the thing that you want to pursue!
Luka mwinjili
alitafuta kwa tafiti kujua moyo wa injili na habari za Yesu. Alitafiti kabla ya
kuandika, alitafiti kabla kuamini na kuwaaminisha wengine. Aliandika baada ya
kupata kujua usahihi wake: “nimeona vema mimi nami, kwa kuwa
nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa
taratibu, Theofilo mtukufu,” Luka 1:3
Kama unataka
kufanikiwa katika siasa jitahidi kusoma na kufanya tafiti ili kujua usahihi wa
siasa. Kama unataka kufanikiwa katika ndoa lazima ujue usahihi wa ndoa, vivyo
hivyo katika ugunduzi na uvumbuzi, uimbaji, uinjilishaji na kadhalika. Wakati mwingine walioko katika medani hizo
watakupa kuujua undani wake kama utakaa nao vizuri. Wengine wako Ulaya ila
kupitia vitabu vyao na kaseti zao unaweza kukaa nao na kujua usahihi wa tasnia
zao. Kwa vitabu mimi hukaa na Benny Hinn, Mike Murdock na Jimmy Swaggart.
Kila siku
binadamu anafanya maamuzi (hutumia akili) zaidi ya elfu tatu (3000) lakini kwa
sababu mengi ni ya mazoea si rahisi kugundua kwamba akili kubwa imetumika.
Tunapanga tuvae nini, tule nini, twende wapi, tufanye nini na nani na wapi.
Maamuzi haya
madogo na mazoea hayatujengi sana kwa kuwa hayushughulisha sana akili
ukilinganisha na kufanya tafiti, uvumbuzi na ufumbuzi wa matatizo. Kila mtu
amezaliwa kutatua tatizo fulani kwa haiba yake, mwonekano wake na vionjo vyake.
Ndio maana si vizuri kujaribu kumuumba upya mtu ambaye tayari amesha umbwa na
BWANA Mungu.
Hivyo ulivyo unafaa
kwa kutatua jambo fulani katika jamii yako, shuleni kwako, au kazini kwako.
Mkimya anafaa kwa uongozi wa ngazi ya sera, “policy level” kama Musa, wakati
msemaji anafaa kwa utendaji wa kila siku kama Haruni. Kwa hiyo tunawahitaji
watu wa vionjo vyote, maandiko yanasema watu wakali humiliki mali, they are strict!
Ile kwamba
unafanya maombi haina maana kwamba, usipime, usifanye utafiti, wala haina maana
kwamba usipeleleze taarifa za hiyo biashara, za hiyo kazi, au za huyo mtu. Ile
kwamba umeomba haina maana kwamba, usiulize waliokutangulia katika tasnia hiyo,
ile kwamba unaimani haina maana usisome. Use
your brain to trace and investigate! Kuna nyakati nilikataa kufanya kazi
kwenye ofisi za tumbaku kwa akili ya kawaida tu, kwamba wanauza saratani.
Matokeo ya sigara ni saratani kwa hiyo kama mkristo sikuwa na haja ya kufanya
maombi bali kutumia akili tu kujua matokea.
Mungu hajaondoa
wala hajasitisha matumizi ya macho, masikio, pua, mdomo na ubongo. Kuna nyakati
nyingine fahamu za mwanadamu ziko sahihi wala huhitaji maombi hapo. Ndiyo, “God does not set aside our natural faculties”.
Tukutane
kileleni …………. usikose msimu wetu wa tano.
0 comments :