Ububu wa Zakaria
UBUBU WA ZAKARIA.
(Bora asiyesema, kuliko anenaye yasiyostahili)
(Bora asiyesema, kuliko anenaye yasiyostahili)
Kuzaliwa kwa
Yohana mbatizaji kulikuwa kwa muujiza, maana wazazi wake walikuwa wazee sana na
wenye kukoma katika kawaida za wanadamu. Zakaria aliposhindwa kuamini
aliyoambiwa na BWANA alifanyika bubu. Kumwacha mwenye imani ndogo azungumze
kunaweza kuharibu ushuhuda, hivyo ni bora afanyike bubu. Talk Faith! Luka 1:20
Biblia inasema
Zakaria alifanywa bubu kwa sababu hakusadiki neno la Mungu (Luka 1:20). Asiye
na imani hutamka mashaka wala hakuna uhai na uwezo wa kujenga katika maneno
yake. Tumepewa vinywa kwa ajili ya kujibariki na kuwabariki wengine. Tumepewa
vinywa kwa ajili ya kumkiri Mwokozi wetu na kuwajenga wanaotusikia. Kwa nini
kuongea jambo ambalo ndani yake hamna tumaini, kwa nini kuzungumza jambo ambalo
ndani yake imani tena ya nini tutamke lile ambalo si faraja.
Akiwajenga
watoto wake mchungaji mmoja alisema, “Talk
love, talk faith, talk hope and edify others” yaani, zungumzeni upendo,
imani, tumaini na kuwajenga wengine. Ni afadhali ukae kimya kuliko kujilaani au
kujiita mdhambi. Tunahesabiwa haki kwa maneno yetu, hatusaidii sana kujiita
wenye dhambi, na kujiona watu duni.
Kristo
alitimiza amri kumi hivyo kupitia Kristo kila aaminiye ametimiza amri kumi
ndani ya Kristo. Hivyo basi si mara zote unapojiita mdhambi unapata rehema,
kuna mara nyingine unajihukumu kwa sababu tu hauna imani ya kujiita mwenye
haki.
John F Kennedy
aliyepata kuwa Rais mwenye upekee wake nchini Marekani alisema, “The only reason to give a speech is to
change the world” yaani “sababu pekee ya kutoa hotuba ni ili kuubalisha
ulimwengu wetu” yaani kuufanya uwe bora zaidi na uwe mahala salama zaidi.
Hatuongei ili
kufanya watu wapigane, hatuongei kuleta uchochozi. Yesu alipotukanwa hakujibu
chochote badala yake alijikabidhi kwa Mungu. Aliamini Mungu anaweza kujibu
mashambulizi hayo vizuri kuliko yeye. Tatizo wengi wetu hatumwamini tunaona
tunaweza kujibu na kulipiza vizuri kuliko Yeye. Tunasahau kisasi ni juu ya
BWANA na kwamba BWANA ni hodari wa vita.
Wako wale
wasemao jino kwa jino au jicho kwa jicho, lakini sheria hii haiwezi kutekelezeka
ikiwa aliyekutendea yu na nguvu kuliko wewe. Waefeso sita imeiita imani yetu
silaha, imeiita pia maombi yetu silaha, kwayo tunaweza kushindana vema kuliko
kwa matusi, dharau na majigambo.
Mungu akubariki
sana!
Usikose msimu
wa tano wa Weekend Purpose.
0 comments :