Bado hujawa tayari kuoa
BADO HUJAWA TAYARI KUOA.
(MANENO YAKO YANAAMUA HATMA YAKO)
Si rahisi
kufahamu mtazamo wa mtu kama hajatamka chochote, si rahisi kujua mawazo ya mtu
asipoyaweka katika maneno. Maneno yetu huonesha hatma yetu. Your words determine your reach!
Maneno yetu
huelezea msimamo na uelekeo wetu juu ya jambo fulani. Kuna baadhi ya maneno mtu
akitamka unaweza kujua hali inayojiri moyoni mwake. Yafuatayo ni baadhi tu ya
maneno yanayooenesha kwamba mtu hayuko tayari kwa kuolewa au kuoa.
Wanawake wote ni sawa. Kitendo cha kusema wanawake wote ni sawa ni hatua inayo onesha mtazamo
mbaya dhidi yao. Kwambo wote ni waovu, au wote hawafai. Mtu mwenye mtazamo huu
hafai kwa kuoa. Hata biblia imetanganisha wako iliyowaita mke mwema na kuna
wengine imewaita kahaba. Wako wazuri na wema kama Abigaili, na unapaswa
kumwomba BWANA ili upewe mke mwema. “Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa
kupata mapato. Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake.” Mithali
31:11-12
Mwanamke atanisaidia nini? Mtu anayefikiri anajitosheleza mwenyewe (self centered and self consumed) na asingehitaji msaada wa mwingine
hafai kwa kuungana naye. Kama hauoni umuhimu wa nafasi ya mke katika kukusaidia
kibiblia na kijamii basi usioe. Ni yule anajua umuhimu wa nafasi fulani ndiye
anayeweza kuipigania hata nyakati za changamoto kali. Ni Mungu aliyesema, Si
vema mwanaume awe peke yake, wala si mwanadamu aliyenena hayo. Kama haikuwa
vema pale Edeni basi ujue si vema hata sasa uwe peke yako. Mwanzo 2:18
Wanawake hawaokoki. Hili nalo si jambo jema. Nimewahi kumsikia rafiki yangu mmoja akilisema na
akinukuliwa na rafiki yangu mwingine. Rafiki yangu huyu ameoa mwaka jana,sasa
sijui kwa nini kaoa. Katika ndoa mwanamke ni kama udongo ambao mwanaume
anapanda maisha yake (Sow your life)
na kinyume chake kwa wanawake. Asiyeokoka maana yake asiye zaliwa mara ya pili
au asiyeamini, Sasa kwa nini upande maisha yako kwa mtu asiye amini? Ingawa
wanaume huwa na msimamo imara sana katika imani na maamuzi lakini bado wokovu
si swala la kijinsia bali ni swala la imani. Luka 8:4
Ataniharibia huduma? Naamini uharibifu katika muungano unaweza kufanywa na mtu yeyote
aliyesehemu ya muungano huo. Kusema ni upande fulani tu si sawasawa, kwani kwa
kufanya hivyo upande mwingine unakuwa ni kama upande wa Malaika. Ni jambo jema
kama pande zote zitalenga na kujizatiti kusaidia mafanikio ya kiroho ya upande
mwingine kiroho. Mithali 31:11-12
Tunakuwa salama
sana pale ambapo fikra zetu zinakuwa sawasawa na neno la BWANA. Pale
tunapowaona wengine ni bora kuliko sisi tunaonesha ukomovu wa akili na imani.
Tunakuwa wenye hekima sana tunapoacha kuwahukumu watu kwa rangi zao, jinsia
zao, kabila lao na nchi zao. Imeandikwa “wote” yaani nchi zote, makabila yote
na lugha zote. Warumi 3:23 “Kwa sababu wote, wamefanya
dhambi na kupungukiwa na utukufu”
Tukutane katika
msimu wa tano wa “weekend of purpose” hapo mwezi May jitahidi ufike, yako mengi
mazuri yanaandaliwa kwa ajili yako mteule wa BWANA. Barikiwa.
0 comments :