Watu wake ni akina nani?
WATU WAKE NI AKINA NANI?
“Basi, kabla ya
sikukuu ya Pasaka, Yesu, hali akijua ya kuwa saa yake imefika, atakayotoka
katika ulimwengu kwenda kwa Baba, naye ali amewapenda watu wake katika
ulimwengu, aliwapenda upeo.” Yohana 13:1
Unaposoma maandiko kwamba, Yesu
aliwapenda watu wake swali unaloweza kujiuliza ni hili, watu wake ni akina nani
hao? Ni kwa nini awapende kwa upendo wote. Neno aliwapenda upeo lina maana
aliwapenda kwa upendo wote au kwa utimilifu wa upendo. Upendo huu Yesu
alionesha wakati mauti yake imekaribia, alipata shida kuachana na wale
aliowapenda na alitamani kuendelea kukaa
nao kwa kitambo kirefu. Ni kama mtu anapotoa wosia wa mwisho kwa watoto
aliowapenda mno.
Katika tafakari yangu ninaamini walio
wake ni hawa:
- ~ Ni wale walioacha vyote wakamfuata [Mathayo 9:27].
- ~ Ni wale waliojikana na kuchukua msalaba [Marko 8:34-35].
- ~ Ni wale waliaminio jina lake [Yohana 1:12].
- ~ Ni wale waliokaa katika neno lake [Yohana 8:31-32].
Makundi hayo manne ni makundi ya watu
ambao BWANA aliwapenda upeo wala hakupenda kuachana nao. Walikuwa watu waliochukua
msalaba na kumfuata, walikuwa watu wenye kusikia neno lake na kulitenda. Hawa ni watu walioacha mashamba, ndugu wa kike
na kiume, ni ambao waliacha mambo mazuri wakaamua kumfuata BWANA.
Sharti la kuwa mwanafunzi wa Yesu si
gumu wala huhitaji kuwa myahudi ili uwe mwanafunzi wake, unachohitaji kukifanya
ni kukaa katika neno lake. Kulisoma kila siku na kulitenda. Ni vema kutenga
muda ili kupata wasaa angalau nusu saa ya kusoma neno na robo saa ya kutafakari.
Kama alivyowapenda waliomwamini nyakati
zile, ndivyo anavyowapenda waamini wa leo, waliaminio Jina lake hata sasa.
Anatupenda kwa upendo wote tena kwa upendo mtimilifu.
Mungu akubariki tukutane Boko Karmeli kwa
masista kwa ajili ya programu ya Weekend of Purpose itakayofanyika Jumamosi na
Jumapili, tarehe 15 na 16 mwezi wa kumi . Usikose
0 comments :