Nataka kuwa kijana milele

6:19:00 PM Unknown 0 Comments

 
NATAKA KUWA KIJANA MILELE

“Forever…. Forever… I wanna be young”, “Milele… Milele… nataka kuwa kijana” Ni kibwagizo katika chaneli ya vijana wa Afrika Mashariki yaani East African Tv maarufu kama Chanel  Five. Kibwagizo hicho kinaonesha wazi namna vijana wanavyopenda ujana na hawako tayari kumaliza maswala ya ujana kwa haraka. Watu wengi wanatamani kurudi utotoni na wazee vijana wanaongezeka kila kukicha.
Msanii mmoja anasema, “ni binadamu peke yake ambaye hukaa na watoto wake kwa zaidi ya miaka kumi na nane.”  Viumbe wengine hawalei kwa kitambo kirefu, wanawajengea watoto wao uwezo wa kujitegemea mapema na kisha wanawatenga. Tai hakai na makinda yake kwa miaka kumi, hata wanyama wa kufugwa hawafanyi hivyo.
Vijana wengi leo si washirika wa maendeleo. Wamejikita katika burudani na michezo isiyo na tija. Wengi wanajaa katika mabanda ya video ili kutazama mechi na  kucheza michezo ya ku-beti. Kundi kubwa la vijana ni watazamaji wa maendeleo. Wanatumia kuliko kuzalisha, wanaisha bila tafakuri ya maisha. Tunahitaji kukua!
Wengi wanachangamkia yasiyofaa, wanajitahidi kufanya yasiyotakiwa. Vijana wamefanikiwa katika mambo yasiyo na tija. Maneno ya Francis Chan ni dhahiri:  “Our greatest fear should be of failure but of succeeding at things in life that don’t really matter”
 Vijana wengi waliofanikiwa wanasifa zifuatazo:
  1. Wametoa changamoto katika magumu yaliyo wakabili. Kila kijana anapaswa kuleta utatuzi dhidi ya dhahma inayomkabili. (Challenge your status quo-the mess your in) Ili kujipima mchango wako katika jamii kama kijana ni lazima uone namna ulivyopambana na mazingira mabaya yanayokukabili. Inaweza ikawa ni ombwe la umasikini, talaka, rushwa, uongo, mmomonyoko wa maadili na kadhalika
  2. Wanahoji. Wengi waliofanikiwa ni waliothubutu kuhoji kuhusu kuvuja vuja kwa imani ya dini yao, kuvuja vuja kwa maadili ya viongozi, kushuka kwa uchumi na hata kutaka kujua sababu zinazopelekea mambo fulani fulani katika jamii yawe kwa namna yalivyo.
  3. Waliofikiri kuhusu kesho. Vijana wanaofanikiwa ni wanaosumbukia hatima zao za baadaye kuliko mambo ya leo. Biblia inasema, “mwana mwenye hekima huweka akiba ya baadaye lakini mpumbafu hula vyote”
  4. Wanajali umilele wao. Ili kukaa na Mungu daima Mbinguni ni lazima kuhusiana naye daima hapa duniani. Kijana mwenye hekima anapaswa kujali mambo ya milele kuliko ya kisasa. What is eternal matters much than what is current!
  5. Wenye ujasiri. Umewahi kuwaza ni mambo mangapi ungetimiza kama usingeliogopa? Ili uende mbele lazima uanze leo. Ogopa kuogopa. Kijana ni mwenye nguvu, mwenye nguvu akiogopa hakuna atayethubutu. Mark Twain Yule mshairi maarufu aliandika: “The secret of getting ahead is getting started”
Mpaka wiki ijayo…Shallom!!1

0 comments :

Fikra sahihi kuhusu Mungu

5:36:00 PM Unknown 0 Comments


 
FIKRA SAHIHI KUHUSU MUNGU
(Orthodoxy) 
Nadhani tumewahi kusikia neno ‘orthodoxy’, likimaanisha usahihi. Lakini kwa somo hili naomba litafsiriwe kama fikra sahihi kuhusu Mungu. Fikra sahihi juu ya Mungu ziko nyingi lakini nitajaribu kuzifupisha katika aya moja. Mungu ni mmoja katika nafsi tatu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Mungu ni wa milele tena ameumba mbingu na nchi. Mungu ameumba vitu vyote vinavyoonekana na visivyo onekana na sisi wanadamu ni kazi ya mikono yake. Mungu ametukomboa wanadamu kwa kumtuma mwanaye pekee mpenzi Yesu Kristo katika umbo la binadamu.
Hizo ndizo fikra sahihi kuhusu Mungu, tukiwaza hivyo tunamuwazia vyema. Anazo sifa za ziada pia kwa uchache ni hizi zifuatazo. Mungu ni mwanzo tena mwisho, Mungu ni Mtakatifu, Mungu ni wa rehema na ni mwenye huruma, Mungu hughairi mabaya tena Mungu ni wa upendo.
Dhana dhaifu kuhusu Mungu (wrong thinking about God)
  1. Wametokana na nyani; Wanasayansi wachache (minority) wanakataa ukweli kwamba, tumeumbwa na Mungu. Hawa si wafuasi wa ‘orthodoxy’. Kwa haraka unaweza kudhani kwamba wanasababu yenye mashiko au wanaye mtu bora ambaye ndiye chanzo cha wanadamu. Nasikitika kuandika, wanadai wametokana na nyani. Yaani, sayansi yao ikiisha kumkataa Mungu inamchagua nyani. What a tragedy! Nimeogopa kuandika ‘tumetokana na nyani’ badala yake nimeandika, ‘wametokana na nyani’ yaani hao wanaoshikilia uongo huo. Hawa tunawaombea ili wajue wazi Mungu ndiye Baba yetu na muumba wetu. 1Yohana 4:4
  2. Hakuna Mungu; Wako wengine ambao Biblia inawaita wapumbavu, hawa wamesema hakuna Mungu. Hawa wanakana uwepo wake. Walipoomba pasipo imani, walipoomba pasipo saburi wakaona hawajapata majibu wakasema moyoni mwao hakuna Mungu. Hawa maandiko yanasema ni wapumbavu (Zab 14:1). Mwl. Mwakasege ananukuliwa akisema; “Mungu ni Mungu hata asipojibu maombi yako.” Anayasema haya katika msiba wa Sedekia ambaye licha ya watu kufunga na kuomba bado Mungu alimpenda zaidi. Zaburi 14:1
  3. Mpinga Kristo: Hawa ni wale walioshindwa kuelewa jinsi Yesu alivyoonekana katika ubinadamu. Hawa hawakupata neema ya kumwamini Mungu pamoja nasi yaani, Emanueli. Wanadai Mungu hawezi kuonekana katika ubinadamu. Hawa wanasahau kwamba, Mungu amewahi kuonekana katika moto (mlimani Sinai), Katika kichaka kinachowaka moto bila kuteketea (alipomtokea Musa) tena aliwahi kuwaongoza wana wa Israeli katika wingu na nguzo ya moto. Sasa kama Mungu ameonekana katika maumbo hayo kivipi ashindwe kuonekana katika umbo la mwanadamu? Dawa ya roho hii ya mpinga Kristo ni imani na ukiri wetu kwamba Yesu Kristo ni Bwana. Ni ujasiri wetu kwamba, Yesu Kristo ni mwana wa Mungu na ni mwokozi wetu. 1Yoh 4:3
  4. Wasio jali wokovu. Hawa wako bize na mambo yao, hawajali mambo ya imani; unaweza kuwaita wapagani. Hawa hawayajui maandiko na hawataki kujua, hawamjui Mungu na hawataki kumtafuta. Hawa wanamuhitaji muhubiri kwani, hawakubali ‘orthodoxy’ wala hawapingi. Hawa mambo ya msalaba wa Yesu ni upumbavu, wanatabia ya wale Wagiriki wasomi wa nyakati za Paulo, ambao kwao msalaba ulikuwa ni upumbavu. Wao usiwaambie kuhusu damu ya Yesu, ni afadhali uwaambie kuhusu vikoba, mikopo ya benki, mitihani ya bodi na kadhalika. Wanasahau usemi huu, “sanda haina mifuko” yaani, utakapokufa hautakwenda na pesa mifukoni wala PHD kichwani. 1Kor 1:18
Rai yangu kwako ni tumwamini Mungu mkuu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Yesu Kristo ambaye Baba alimtuma ili atukomboe. Chukua nafasi hii kugeukia usahihi ikiwa uko katika kundi lolote kati ya hayo. Kitendo cha kuwepo kwenye kundi moja kati ya hayo manne kinatosha kukupeleka jehanamu ya moto hata kama haupo kwenye makundi mengine matatu. Tutubu na kuiamini injili. Tutembee katika usahihi. Right thinking about God!!!!

0 comments :

Sitaki kukosa baraka hizi

12:28:00 PM Unknown 0 Comments

 
SITAKI KUKOSA BARAKA HIZI
Ilikuwa mwezi Desemba 2015 nikiwa katika basi la Mbeya Express kuelekea Mpanda huko Katavi. Kama ilivyoada nilikuwa na kitabu changu mkononi ili kurahisisha safari yangu. Na katika mapumziko hayo mafupi ya siku kuu ya Chrismas niliamua kuchochea uinjilishaji kwa kusoma kitabu hicho cha mwandishi Marc Cahil, “One Thing You Cannot Do In Heaven”
Kitabu kinahusu uinjilishaji tena si rahisi kukutana na ujumbe mwingine katika kitabu hicho ambacho nilikuwa nakisoma kwa mara ya pili. Wakati huo hali yangu ya uchumi ilikuwa si nzuri, ingawa nilikuwa nakwenda likizo nilikuwa nakwenda nikiwa na wazo la kupunguza matumizi. Nilikuwa natembea nikiwa na tahadhari kichwani, ya kupunguza matumizi hususani ya fungu la kumi. Ghafla ndani ya kitabu nikakutana na onyo, “Unapotaka kupunguza matumizi usipunguze pesa ya sadaka au fungu la kumi”
Yaani, unaweza kupunguza matumizi ya nguo; chakula, vinywaji, safari na mengine lakini si matumizi ya sadaka na zaka. Niliposoma ujumbe huo nikaweka azimio moyoni kwamba sitapunguza matumizi ya zaka badala yake nitatoa kama ilivyokawaida 10%. Ilinisumbua kidogo kwani nilikuwa nimepanga tayari kupunguza matumizi ya sadaka ili kumudu mambo mengine.
Mwandishi alinukuu maandiko kutoka katika Biblia jinsi Mungu atakavyo fungua madirisha ya mbinguni na kunibariki hata isibaki nafasi, nilisoma pia namna atakavyo nilinda na kuondoa hali ya kuvuja kiuchumi. Baada ya kuzisoma ahadi hizo niliandika pembeni ya kitabu maneno haya, “siko tayari kukosa Baraka hizi” yaani, “I am not ready to forfeit these blessings.”
Nilipofika nyumbani niliamua kumtolea Mungu bila kupunguza kiwango licha ya changamoto iliyokuwapo. Nilipomtolea Mungu alinibariki mno tena kwa haraka akinipa zaidi ya mara tano ya sehemu niliyotoa zaka ndani ya siku saba. Kila ninapotoa fungu la kumi ninamwona Mungu. Mara nyingine umeme uliachiliwa pasipo kupoozwa vema na watu wengi walishuhudia uharibifu wa mali, jirani yangu pia alishuhudia vitu vyake vikiungua. Asubuhi wakati ananipatia taarifa ya kilicho tokea ndipo nilisikia ndani yangu Roho akinikumbusha lile neno kwamba, tukitoa zaka kamili Mungu atamharibu yeye aharibuye. Nami nikajua wazi ni Mungu aliyeokoa vitu vyangu kutoka katika uharibifu wa umeme. Asubuhi hiyo niltamani niwashuhudie jirani zangu kwa nini Mungu amelinda vitu vyangu lakini sikupata kibali kwani wangeweza kutafsiri kama majigambo ilhali ni shauku yangu kuona wengi wanakata bima kutoka mbinguni kwa njia ya fungu la kumi.
Mtu pekee ambaye anachukia kutoa fungu la kumi ni yule ambaye hawajawahi kutoa na hivyo hajaonja baraka za kutoa zaka. Kwa sisi tulio onja kwa kweli, hatuwezi acha tabia hiyo. Anthony Robbins anashauri watu kuweka akiba moja kwa moja lakini mimi nashauri tutoe zaka moja kwa moja.
Hata kama matumizi yako yameongozeka epuka kuacha kutoa fungu la kumi kwa sabau tu eti matumizi yameongezeka. Toa hata katika hali ya shida. Tahadhari! Wengi wametoa na huenda hawajaona Mungu akitenda kama nilivyoshuhudia. swali langu kwao, walikwenda kutoa sehemu gani? Nimewahi kuulizwa, “Ni wapi nikatoe fungu la kumi?”
Katoe mahali unapolishwa kiroho, toa mahali wanapoliheshimu neno la Mungu, toa kwa wale wanaotaabika kwa ajili ya kuwalisha watu chakula cha roho yaani neno. Chunguza udongo na kisha toa kwa watumishi waadilifu. Mkulima anapaswa kuchagua udongo, hali kadhalika tunapotoa zaka, sadaka na dhabihu lazima tuchague udongo. Eneo unalopeleka zaka litakupatia neno kwa wingi, ukichunguza utaona maeneo mengi ambayo watu hawatoi zaka hakuna neno. Mungu alisema tutoe zake ili chakula (neno lake) liwe kwa wingi ghalani (Kanisani/fellowship/huduma na nk).

0 comments :

Mpaka umevuka, hakuna kusogea..!

10:14:00 AM Unknown 0 Comments

 

MPAKA UMEVUKA HAPA, HAKUNA KUSOGEA...!
Wakati yupo shule (akiwa mdogo), aliyewahi kuwa kiongozi mashuhuri Dr. Myle Munroe; alikuwa mwanafunzi wa mwisho darasani katika kila matokeo. Kwa wakati ule hakuna aliyefikiri angeweza kufanya jambo lolote la maana; si tu ulimwenguni lakini hata katika maisha yake binafsi. Anasema siku moja wakati anasoma biblia alikutana na na sehemu inayosema, “Nayaweza mambo yote katika Yeye (Kristo) anitiae nguvu”; na hapo ndipo ulipokuwa mwanzo wa maisha yake kubadilika pamoja na mabadiliko kimasomo; kwa wastani wa mwaka mmoja alitoka kuwa mwanafunzi wa mwisho darasani hadi kuwa mwanafunzi bora shule nzima, mpaka anamaliza.
Mpaka tumefikiri sawasawa, hatuwezi kuishi sawasawa. Mawazo yaliyopata nafasi ndani ya mtu juu ya jambo fulani au eneo fulani la kimaisha, ndiyo yatakayoamua hatima yake katika eneo hilo. Kama mtu hajaridhika na hali fulani katika maisha yake; njia ya pekee na ya kudumu ili kutoka mahali hapo, ni kwa kukutana na wazo mbadala litakalo zaa matumaini kwa kumpa kuona picha iliyobora zaidi anayopaswa kuifanyia kazi.  Mwanadamu atabaki katika hali hiyo hiyo aliyopo mpaka wazo mbadala limeingia na kutawala katika kichwa chake (Exposure).
Kama tunataka kuwa na matokeo tofauti na watu wa kawaida (average people) au tofauti na wakati uliopita katika eneo fulani; ni lazima tufikiri na kufanya tofauti. Kama haulidhishwi na kiwango cha kimaisha au kiroho ulichopo sasa; hali hiyo ya kutokuridhika unayoisikia ndani yako ni wito wa kukutaka ufikiri na kufanya tofauti na unavyofanya sasa.  Mwanasayansi Albert Einstein amewahi kusema, “Ni uendawazimu; kufanya kitu kile kile kwa namna ile ile, na kutegemea kupata matokeo tofauti” (Tafasiri isiyo rasmi)
Hakuna mtu anayeweza kwenda mbali zaidi ya mawazo yake aliyonayo sasa; mpaka umeelewa jambo hili, mambo hayawezi kusogea. Isaac Newton, “mwanafisikia” katika kanuni yake ya kwanza (Newton’s first law of motion) anasema, “Kitu kitabaki katika hali yake hiyo hiyo iliyopo, mpaka imekutana nguvu kutoka nje” (Tafasiri isiyo rasmi)
Mwandishi wa karne ya kwanza Paul katika kitabu chake kwa wafilipi anatoa vigezo vya kuzingatia unapochagua aina ya mawazo yanayopaswa kupata nafasi na kutawala ndani yako; akiwa na maana kwamba, endapo wazo halitakuwa na sifa au vigezo hivyo, usilipe nafasi ya kufanya makazi ya kudumu katika moyo [akili] wako.
Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya staha, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote. Yatafakarini hayo. Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia na kuyaona kwangu, yatendeni hayo...” Wafilipi 4:8-9 (Msisitizo umeongezewa)

0 comments :