Umuhimu wa kutambua kusudi - II
Tofauti kati ya
Kusudi (Purpose) na Maono (Vision)
Kusudi maana
yake ni sababu iliyofanya au inayofanya kilichopo kiwepo au kitengenezwe jinsi
kilivyo (design) ili kutimiza kazi maalumu; katika kufikia malengo yaliyokuwa yamekusudiwa
awali kabla ya kitu hicho kuwepo au kutengenezwa.
Kusudi ni kongwe
kuliko mtu au kitu husika. Kusudi huishi moyoni mwa msanii au muumbaji kwa muda
mrefu. Mtu hapangi kusudi lake kwa kuwa halitoki akilini mwa mtu, bali hutoka moyoni
mwa Mungu muumbaji. Haulichagui bali unaweza kuligundua. Lipo kabla ya mtu, ni
kazi ya mtu kulijua. Mark Twain mshairi mwenye alama ya aina yake ulimwenguni amewahi
kusema kwamba, “Siku mbili muhimu kwa mtu ni siku aliyozaliwa na siku
aliyogundua kwa nini amezaliwa.”
Neno
maono linawezakuwa na tafasiri
nyingi; lakini kwa makusudi ya somo hili, Maono maana yake ni picha ya kusudi
inayowekwa wazi/kufunuliwa (revealed) ndani ya moyo wa mtu. Kusudi la kitu/mtu
linapojulikana na mtu huyo ndipo huitwa maono. True vision is born when purpose is known.
Kusudi linaonesha
sababu ya kuwepo kitu; Na kusudi hilo linapojulikana au kuwekwa wazi ndipo
huitwa maono. Hivyo basi, Maono ni
kusudi lililowekwa wazi na kujulikana ndani ya moyo [mind] wa mtu.
Kusudi huonesha
hali ya mwisho wa jambo/kitu/mtu, jinsi anavyotakiwa au anavyopaswa [kusudiwa]
kuwa kulingana na malengo ya aliyefanya jambo hilo au kitu hicho kuwepo. Maono
huonesha picha hiyo ya mwishoni mwanzoni; maono huonesha picha ya kusudi iliyo
mbele mwanzoni ili mtu apate kuiendea kwa ujasiri na kuwa na uhakika wa
kuifikia picha hiyo kwa maana ni Mungu ameadhimia iwe hivyo. Inakupa kujua
mwisho wa safari kabla ya kuanza safari. [Isaya 46:9-11]
Kusudi la
kitu/mtu huwepo kabla ya kuumbwa kwa mtu; kusudi hilo hufunuliwa na kuwa maono
[ndoto, njozi] kwa msaada wa Roho Mtakatifu [Yoeli 2:28]. Bila ya Roho
Mtakatifu kututambulisha kusudi la Mungu, maisha hujawa na majaribio. Maono ni
tunda la mahusiano na Mungu, kwa kadiri unavyohusiana naye ndivyo anavyozidi
kukufunulia na kukuonesha maono yako hatua kwa hatua. [Mwanzo37:5-11]
Kusudi
halihitaji umjue Mungu; ile kwamba umeumbwa tu lenyewe lipo, hata kama humjui
Mungu na hutaki kumjua. Wengi wamekufa pasipo kuona maono kuhusu maisha yao yaani,
pasipo kujua wameumbwa na kuletwa duniani kwa kusudi gani. Maono ya kweli
yanahitaji uwepo wa Mungu katika Roho Mtakatifu ili kukuwezesha kuyajua. [1Kor
2:11-12]
Mfano
mzuri ni Mtume Paulo, katika Galatia 1:13-16 na Matendo ya Mitume 9:6, 15-18.
Kumjua YESU kama Bwana Na Mwokozi wa maisha yako, hakukupi tu uhakika wa maisha
yako bada ya kufa, lakini pia unapata fursa ya kuishi maisha yenye ufanisi na kuleta
maana hapa duniani.
See you at the top
0 comments :