Baada ya kulitambua kusudi la kuumbwa kwako
Ukishafikia
hatua ya kutambua kusudi la Mungu juu ya maisha yako hatua zifuatazo ni muhimu
sana:
- Liandike
Ni
muhimu sana kila mtu kuandika kusudi lake au maono yake katika aya yenye
sentensi chache iwezekanavyo. Hii itakusaidia kulikumbuka daima kila unapoona
sentensi hiyo na kukupa nguvu ya kuiendea hadi mwisho [Habakuki2:2—3].
“Ni vizuri kuibandika karatasi hiyo inayoelezea picha ya maono ya maisha yako ya baadae [kwa ufupi], chumbani au mahali popote pa wazi ili kila uisomapo uweze kukumbusha na kukuhamasisha”
Nimewahi
kusoma mwandishi mmoja ambaye yeye anashauri sentensi hizo zisizidi tatu, lakini kwa maoni yangu si
mbaya hata zikifika tano. Tazama kusudi la Yohana mbatizaji lilivyo katika
sentensi chache. “Palitokea mtu,
ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana. Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa
yeye” Yohana 1:6
Ni
vizuri kuibandika karatasi hiyo inayoelezea picha ya maono ya maisha yako ya
baadae [kwa ufupi], chumbani au mahali popote pa wazi ili kila uisomapo uweze
kukumbusha na kukuhamasisha. Kwa mfano zifuatazo ni sentensi ambazo nimeandika
ili kuelezea kusudi la kuumbwa kwa watu kadhaa ukianza na mimi:
1. “My
purpose is to you use all I have, to give myself into the preaching of the
gospel and inspire others to live for Christ” Alphonce Luhamba’s vision
(purpose) statement
2. “To uplift
humanity consciousness through business”
3. “To
inspire and empower people to live their highest vision in context of love and
joy”
4. “To create
and inspire one million millionaires who each will donate one million dollar to
his or her church charity”
Ni
vema kurahisisha kwa kuandika au kuchora alama zenye kuonesha picha ya kusudi
la kuumbwa kwako. Mchoro huo au maneno
hayo ni lazima yawe yanakuvutia, yaweze kukuhamasisha na kukupa changamoto ya
kuyafanyia kazi katika kutimiza kusudi hilo. [Your
Vision or purpose paragraph must challenge your comfort zone.]
Ni
vizuri kulisoma kusudi lako kila siku, ni vema kuliacha liimbe kichwani mwako
kila dakika. Kama Ilivyokuwa kwa Yohana mbatizaji wewe pia umetumwa na Mungu,
na umetoka kwa Mungu. Haupo duniani kitalii, upo kikazi. Muda wote tuwapo
duniani tupo safarini kwa kazi maalumu. Badala ya Yohana, waweza kuweka jina
lako. “Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa
Mungu, jina lake.....”Yohana 1:6
- Achana na utafiti.
Ukishajua
kusudi au maono yako haunabudi kuacha kujiuliza uliza maswali mengi. Hakuna
haja ya kuogopa. Ni muhimu kudumu katika Neno la Mungu ambalo ndio chakula
muhimu kwa kila mbeba maono na makusudi ya Mungu. Kusudi lako litaendana na
Neno la Mungu hivyo usiache kulisoma.
“Kuachana na utafiti usio na tija kutakujengea ujasiri na uhakika wa kupata ushindi; na matokeo yake Imani yako kwa Mungu juu ya maono hayo itaongezeka”
Katika
kusudi ushindi lazima. Kuachana na utafiti usio na tija kutakujengea ujasiri na
uhakika wa kupata ushindi; na matokeo yake Imani yako kwa Mungu juu ya maono
hayo itaongezeka. Achana na maswali ya nitaweza au sitaweza, Mungu aliyekuita
atakuwezesha. Tunapokuwa katika kusudi la Mungu tuna uhakika na ushindi wala
hatubahatishi.
Baada
ya kuachana na maswali, unapaswa kubaki na maneno machache tu ya ushindi.
“Nitaweza na nitafanya na nitakuwa vile ambavyo Mungu anataka niwe. Unapaswa
kusema kama Daudi, Sitakufa mimi bali nitaishi, ili kufanya kazi niliyoitiwa na
BWANA.
- Litende na kuimaliza kazi kwa gharama yoyote ile.
Kwa
sababu ya hofu ya kulipa gharama mara kadhaa utajikuta katika nafasi ambayo ni
rahisi kufanya kila kitu isipokuwa kusudi la kuumbwa kwako, hata hivyo unapaswa
kulichagua kusudi lako hata kwa mateso. “Chakula change ndicho hiki niyatende
mapenzi yake yeye aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake…”Yohana4:34. Jim Rohn
anaandika, “Kama una nia ya kutaka
kufanya jambo, utatafuta njia ili kulifanya; kama huna nia, utatafuta
visingizio kwanini hauwezi kufanya” (Tafasiri
isiyo rasmi)
Gharama
inaweza kubwa lakini ni muhimu kuhakikisha kwamba kusudi linatendeka, maana
gharama huakisi uzuri wa taji yako. Gharama inawezakuwa ya juu (steeper) kama
vile: Kuacha kazi fulani, kurudi tena shule au kutengwa, kujikatalia mambo ya
kidunia, kuonekana mshamba au kukosa muda wa kupumzika. Kusudi la Yesu
lilimnyima hata muda wa kulaza ubavu wake. Ili kufanikisha jambo lenye kuleta
maana duniani mwenye hekima mmoja anaandika, “Hakikisha kazi inafanyika kwa gharama yoyote”.
- Weka na kupanga mipango
Maono
au mipango ni ulinzi wako. Hatuhitaji “body guard” kama Rais, tunahitaji maono
ili kutuokoka katika maangamizi. Mipango mizuri ya baadaye ni ulinzi tosha,
itakuzuia na itakuruhusu pia. Pasipo maono na mipango dhabiti, watu huacha kujizuia na
hivyo huangamia.
Mipango
ni njia ya kuiendee hatima yako. Mipango ni hatua kuelekea katika hatima
iliyowekwa mbele yako kwa sura ya maono [Mithali 16:9]. Ni vizuri mipango yako
ikazingatia muda. Usikubali kubahatisha
au kupangiwa na mtu. Ni vizuri ukaweka mipango dhabiti ili kutekeleza kusudi la
Mungu katika maisha yako. Mipango
inakufanya uone mbele, inakusaidia usirejee nyuma. Mipango inakupatia nafasi ya
kuishi maisha ulikwisha yafikiri. Pasipo mipango au maono watu hurejea nyuma na
hivyo huangamia.
“Watu wanaopenda kufuata mkumbo hawapendi kupanga mipango yao wenyewe, wanaridhika kuwa mashabiki wa watu fulani au wa kikundi fulani”
Ukiwaruhusu
watu wapange kwa ajili yako watakupangia kijisehemu kidogo; tofauti na wito au
uwezo ambao Mungu ameweka ndani. Mipango
ni wajibu wako binafsi usioweza kukaimishwa [delegate] kwa mtu yeyote. Watu
wanaopenda kufuata mkumbo hawapendi kupanga mipango yao wenyewe, wanaridhika
kuwa mashabiki wa watu fulani au wa kikundi fulani. Usipopanga mipango yako,
utaangukia katika mipango ya mtu mwingine; hii haikupi uhakika wa kufikia
kilele cha mafanikio yako.
“Utahitaji kuchochea kipawa chako; na hapa ni muhimu utafute maarifa na ujuzi sahihi ili kukuwezesha kutumia vyema kipawa chako”
- Tafuta maarifa
Wakati
mwingine kusudi lako linaweza kukuhitaji utafute maarifa na weledi wa juu ili
kulitekeleza kwa ufanisi. Utahitaji
kutoka kwenye “kipawa [gift/talent]” mpaka kwenye “ujuzi [Skills]”. Utahitaji
kuchochea kipawa chako; na hapa ni muhimu utafute maarifa na ujuzi sahihi ili kukuwezesha kutumia vyema
kipawa chako. Waweza kwenda shule ya muziki, au utahitaji kwenda shule ya
sheria, au kurudi tena shule hata kama mwanzoni uliishia njiani, waweza kwenda
shule ya Biblia ikibidi, waweza kuwa mfuasi wa mtu mwaminifu aliyefanikiwa katika eneo unalotaka kufanikiwa ili
kujifunza kutoka kwake [mentorship/coaching].
Watu
wengi wenye vipawa hufanana lakini juhudi, ujuzi na maarifa hufanya
watofautiane; inawezekana wote ni waimbaji, lakini mmoja anaimba kwa ujuzi [skills]
na mwingine hana ujuzi huo. Marafiki sahihi, usomaji wa vitabu na utazamaji wa
vipindi vinavyolisha maono yako ni mambo yenye kukupatia msaada na kulifanya
kusudi lako litendeke kirahisi, kwa ufanisi na kwa mafanikio makubwa.
0 comments :