Pasipo Msongo

5:13:00 PM Unknown 0 Comments

PASIPO MSONGO WA MAWAZO - I

[Stress Free Zone]
Katika maisha haya ya sasa watu wengi wanakabiriwa na maswali mengi; na wale wasio na maswali wana majawabu ya uongo yaani, ambayo si sahihi. Lini nitaajiriwa? Lini nitaolewa? Nitavaa nini? Nini itakuwa hatima ya maisha yangu? Ni miongoni mwa maswali tata katika kizazi chetu.
Kwa kuwa ukombozi wa Yesu Kristo unahusisha; mwili nafsi na roho hakuna namna tunavyoweza kuepuka kujibu maswali haya kama viongozi na watumishi katika Kristo. Kwa wanasiasa baadhi ya maswali haya ni mtaji wao wa kuwafikisha katika matarajio yao.

Unayo nafasi

7:34:00 PM Unknown 0 Comments

UNAYO NAFASI YA KUANDIKA HISTORIA YAKO-II
Watu na wafanikiwe kupitia kufanikiwa kwako
Kila mtu ana shauku ya kutaka kujua namna ya kufanikiwa na kumiliki vitu. Vitabu vyenye picha za fedha, majumba na vitu vya thamani huchapishwa, makampuni hufunguliwa na mahubiri hutolewa yakiwa na lengo la kuvutia watu katika kufikia ndoto zao. 

0 comments :

Itifaki ya Upendo

10:24:00 AM Unknown 2 Comments


ITIFAKI YA UPENDO
(Love Protocol)
Mambo mengi katika maisha ya sasa yanazingatia itifaki. Sote tu mashahidi wa jambo hili, mara nyingi katika kutambulisha, ofisini na hata katika ngazi ya familia itifaki huzingatiwa. Jamii nyingi katika chakula ni wazee ambao hutangulia kunawa au kunawishwa mikono yao kwanza kabla ya rika la vijana na watoto. Mahali pengine ni viongozi wa ngazi za juu huwasili mwishoni baada ya kutanguliwa na wale ngazi za chini, na inafahamika wazi kwamba, viongozi wa meza kuu ndiyo hutambulishwa kwanza. Yote hii ni itifaki.
Amri kumi za Mungu zimekaa katika namna au mpangilio wa ki-itifaki. Ukizisoma kwa utulivu utaona kuna itifaki ndani yake. Zinaanza kwa kuonesha kwamba Mungu peke yake ndiye astahiliye kuabudiwa, zinaendelea na umuhimu wa kuheshimu wazazi na kuwapenda, baadaye zinatufunza namna njema ya kukaa na jirani zetu na kuwapenda.
“Alishatoa kila kitu kwa ajili yetu, hivi sasa hakuna kilichosalia mbinguni. Alipomtoa Yesu alitoa kilicho cha thamani kutoka mbinguni”
Leo tunatamani msomaji wetu uijue itifaki ya upendo (love protocol) ambayo ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku. Ni rahisi kabisa, itifaki ya upendo inataka aanze Mungu, ufuate wewe, wazazi na baadaye jirani yako. Mpende BWANA Mungu wako, jipende, na mpende jirani yako kama unavyojipenda.  Mathayo 22:37-39
MUNGU; Ni Baba yetu mwema Yeye alitupenda kwanza, alitupenda upeo. Alishatoa kila kitu kwa ajili yetu, hivi sasa hakuna kilichosalia mbinguni. Alipomtoa Yesu alitoa kilicho cha thamani kutoka mbinguni (Warumi 8:32). Mbele za Mungu Baba, Yesu alikuwa ni kila kitu, ni zaidi ya jinsi Ibrahim alivyompenda Isaka. Lakini kwa ajili yako na yangu alimtoa. MUNGU ndiye anayetutunza, asubuhi hutoka kwake; Yeye ndiye aliyetuumba, tena tu kazi ya mikono yake. Hatuna budi kumpenda kuliko yeyote na kupita chochote. Itifaki ya upendo inadai MUNGU kwanza wengine baadaye. Si vema kujipenda zaidi kuliko kumpenda Mungu. Mpe kipaumbele asubuhi, mtukuze jioni, mtafakari usiku. Mzee Yohana anaeleza vizuri katika 1Yohana 4:10-11: “Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu. Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana.
“Unatakiwa kujipenda kiasi kwamba ikitokea nafasi ya kuumbwa tena uchague kuwa wewe katika rangi hiyo hiyo na urefu huo huo”
WEWE; Mara nyingi tumewakumbatia wale waliotuumiza na kutitirisha machozi kila uchwao, huko ni kukosa kujipenda; huwezi kumpenda jirani yako kama hujipendi. Huwezi kutoa usichonacho. Katika usanii wa hali ya juu ni pale ambapo asiyejipenda anajaribu kupenda, hahaha ni vituko! Kujichubua ngozi kwa vipodozi (kuji-cream) ni matokeo ya kutojipenda. Mtu anayetamani kwenda ulaya hata kuhatarisha uhai wake utadhani pamekuwa Mbinguni ni matokeo ya kutojipenda, binafsi natamani kwenda mbinguni kazi yangu ikiisha. Mungu ndiye aliyeweka mipaka, anasababu ya kufanya uwepo katika nchi uliyopo. Kutamani kuzaliwa mzungu badala ya Mtanzania au Mwana wa Afrika ni kutojipenda pia. Unatakiwa kujipenda kiasi kwamba ikitokea nafasi ya kuumbwa tena uchague kuwa wewe katika rangi hiyo hiyo na urefu huo huo. Usitamani kuwa fulani bali tamani kuwa wewe ambaye Mungu anataka uwe. Kujipenda ni kujikubali hata kama hujavaa nguo fulani, hujazaliwa familia fulani au hujaenda nchi fulani. Ninajipenda kiasi kwamba hujitoa katika mtoko wa jioni, najifurahia, najisemea mwenyewe na ninajiheshimu kabla mtu mwingine hajaniheshimu. Zingatia itifaki jipende tafadhali! Usipate hadhi au kupanda chati kwa sababu umevaa nguo fulani bali nguo ipate hadhi kwa sababu wewe umeivaa.
WAZAZI; Itifaki inataka tuwapende wazazi wetu. Biblia imewataja moja kwa moja kwamba, tunapaswa kuwaheshimu. Wazazi ni lango la baraka, anaweza asikupe mtaji wa biashara lakini maneno yake tu ni “dili”. Kumbuka Yakobo na Esau, walitaka haki ya mzaliwa wa kwanza ambayo hutolewa kwa maneno tu. Nakumbuka siku moja Baba yangu alinipigia simu akaniambia nitafanikiwa kwani, sijachukua cha mtu na nikaamini nitafanikiwa; Ukiniuliza kwa nini nitakujibu, ‘baba kasema’. Japo nasoma maandiko na najua jinsi Yesu alivyotufanikisha kwa Damu yake lakini sipuuzi Baraka ya wazazi. Mwalimu Mwakasege anaandika, “Ukitaka kujua mchumba wako ataishi muda gani angalia anachowatendea wazazi wake.” Sasa kama unataka kuwa mjane mapema si lazima kujua hili. Usisahau hili, heshima kwa wazazi huamua juu ya urefu wa maisha yako hapa duniani. Wasamehe wakikosa, wasikilize wakikuonya, wasaidie kila upatapo nafasi. Wapende.
“Je uko tayari kuvunja uhusiano wowote unaoharibu itifaki ya upendo katika ngazi ya Muumba wako? Je, unaweza kukaa mbali na huyo mtu anayekuwa chanzo cha kuharibu uhusiano wako na Mungu?”
JIRANI; ujirani si habari ya nyumba au ya kuishi mtaa mmoja. Ujirani ni nafasi ya kusaidia. Kila unapokuwa na nafasi ya kumsaidia mtu unafanyika jirani yake. Safarini kuna majirani, barabarani kuna majirani, ofisini kuna majirani, kanisani kuna watu huhitaji msaada pia. Ni ajabu kama hatutatambua hisia na mahitaji ya watu wengine na tukaendelea kujiita wakristo. Ukianguka barabarani ungependa watu wakutendee nini? Siku yako ya kuzaliwa ungependa watu wafanye nini? Ukiugua ungepende watu wachukue hatua gani?  Ukipata msiba ungependa watu wachukue jukumu gani? Ukishindwa masomo ungependa watu wazungumze maneno gani? Ukigombea nafasi ya uongozi na usiipate au ukakatwa, ungependa watu wanene maneno gani? Yale ambayo ungependa ufanyiwe basi watendee na wengine pia. Maneno ambayo ungependa kusikia, wasikilizishe na wengine pia na huo ndio ujirani.
ANGALIZO; Unajua itifaki inaweza kuvamiwa au kuingiliwa, wengine husahau na hivyo kushindwa kuzingatia itifaki. Mahali ambapo baba na mama wapo usianze kuwatambua mashemeji zako kwanza, mahali ambapo mwenyekiti yupo usianze kumtambua mweka hazini kwanza. Wengine hutambua vitu kabla ya watu na utu, wengine hutambua wapendwa wao kabla ya Mungu. Ibrahimu alikuwa tayari kumpoteza Isaka ilimradi itifaki ya kwamba Mungu ni Mkuu izingatiwe. Biblia inasema kidole chako kikikukosesha ukikate, Je uko tayari kuvunja uhusiano wowote unaoharibu itifaki ya upendo katika ngazi ya Muumba wako? Je, unaweza kukaa mbali na huyo mtu anayekuwa chanzo cha kuharibu uhusiano wako na Mungu?
Kuhani hupenda ibada, mwinjilisti hupenda mahubiri, manabii hupenda unabii; heshima ya nabii ni kutimia kwa unabii wake. Lakini Mungu hupenda watu hatulii hadi aone usalama wa viumbe vyake. Yona alivunja itifaki, alipenda unabii wake kuliko watu. Alisikitika kwa nini Mungu hajawaangamiza watu wa Ninawi kama alivyotabiri. Kwake yeye bora watu wafe ilimradi unabii utimie, kwa Mungu bora unabii ubatilike lakini watu waokolewe. Yona 4:1
Yesu alizungumza kwa habari ya kuhani aliyependa ibada kuliko utu. Alimwacha mgonjwa aliyevamiwa na wevi kwa sababu anawahi ibada, huyu naye hakujua itifaki ya upendo. Mungu kwanza, wewe na jirani ndio mnafuata; Karama na vitu huja baadaye, Haleluyah! Itifaki ya ki-kristo inatutaka tuwapenda adui zetu na tuwatakie mema hili nalo si jambo la kubezwa. Tafadhali itifaki izingatiwe na neno la BWANA lizingatiwe kwa vitendo.
Tukutane katika mbingu mpya na nchi mpya.
Naomba kuwasilisha.

2 comments :

Ogopa Kougopa

10:46:00 AM Unknown 0 Comments


OGOPA KUOGOPA
(FEAR To FEAR)

Kuna nyakati Mtunga zaburi amewahi kusema, “Ee nafsi yangu kwa nini kuinama (kufadhaika/kuogopa)”. Ni wazi hakupendezwa na hofu, wala hali ya kutokujiamini iliyokuwa ndani yake. Moja wapo ya sababu kubwa inayofanya watu wengi kushindwa kufikia kilele cha mafanikio yao ni hofu ya kushindwa. Nashawishika kusema, hofu ya kushindwa imewafanya watu wengi kushindwa kufikia mafanikio yao kuliko kushindwa kwenyewe (Fear of failure has failed a lot of people than failure itself)
“hofu ya kushindwaimewafanya watu wengi kushindwa kufikia mafanikio yao kuliko kushindwa kwenyewe”

Hata watu wakuu walikutana na hofu walipoanza kutekeleza majukumu yao. Tofauti yao na watu wengine, ni kwamba hawakuruhusu mashaka na hofu zao kuwa kubwa kuliko picha ya mafanikio iliyokuwa mbele yao (vision); na hivyo walisonga mbele na kufanya mambo makubwa yaliyopata heshima katika vizazi vyao na vizazi vilivyofuata baada yao.  Walijua kuwa picha ilikuwa ndani yao ni halisi kuliko mazingira ya hofu yaliyokuwa yakiwazunguka kwa wakati huo.
Rick Warren amewahi kuandika, “Kila tunaposhindwa, kuna uongo nyuma tuliouamini” (Behind every self-defeating act is a lie you believe); hii ni kauli yenye kuhekimisha. Hofu ni moja ya uongo, hofu hufanya watu washindwe masomo kabla ya mitihani, hupelekea bondia apigwe nje ya ulingo, hofu huua kabla hata mtu hajafumba macho; hofu humpa mtu talaka kabla ya ndoa.
Kuna usemi usemao, “Njia ya muongo ni fupi.” Hofu ni uongo na hivyo njia yake ni fupi. Tunaweza kuiaibisha hofu na kuikamata katika uongo wake kwa kuyafanya yale yanayotutisha. Watu wakuu waliiaibisha na kuikamata hofu katika uongo wake baada ya kwenda mbele na kufanya walioyaogopa kwa Msaada wa BWANA. Hofu hutoweka tunapofanya tunayoyaogopa.   Oh! Mungu akusaidie kupata hisia za Daudi baada ya kumuua Goliathi. Oh Glory…I can feel it, how beautiful it was, to kill what was scared by the whole Nation.
Kwa sababu ya hofu ya kushindwa wapo waliokufa na biashara, makampuni, huduma, sanaa, miradi na vumbuzi mbalimbali (zilizoishia kuwa mawazo na ndoto tu) walizopewa kwa makusudi ya kuboresha maisha ya watu wengi katika vizazi vyao na kwa ajili ya vizazi vitakavyofuata baada yao. Kila mtu ameumbwa kwa kusudi maalumu, na kila mtu anacho kitu cha kuchangia katika kizazi chake na vizazi baada yake; lakini kwa sababu ya hofu, vitu vingi vimebaki kuwa mawazo na ndoto tu katika mioyo ya watu wengi.

Aliyeahidi ni mwaminifu.

Ili kupata uhakika kama ahadi uliyopewa itatimizwa au haitatimizwa, jambo la kuangalia si uzuri wa ahadi iliyotolewa bali mtu aliyetoa ahadi hiyo. Ahadi inaweza kuwa nzuri lakini aliyetoa asiwe na uwezo wa kutekeleza. Ibrahimu alijua siri hii muhimu; hata alipooneshwa picha, ya kuwa katika yeye mataifa yote watabarikiwa, na mazingira yake hayakuonyesha kama jambo hilo litawezekana jambo moja tu alijua nalo ni kwamba, Aliyeahidi ni mwaminifu hakika atatekeleza alichoahidi. Ukweli huu ulinyima nafasi ya hofu kudhoofisha (paralyse) imani yake.
“Watu wakuu walishinda hofu zao kwa kuwa ndani yao walijua picha walionayo ndani ya mioyo yao ni halisi kuliko mazingira yao na tena imani yao haikuwa kwenye ahadi walizopewa bali imani zao waliziweka kwa Mtoa Ahadi”

Mungu anapokupa wazo ulifanyie kazi au maono (vision), mara nyingi mazingira yako hayatalingana na maono hayo. Hofu huwa kubwa pale tunapoacha kuangali ahadi ya Mungu na picha iliyowekwa mbele yetu na kuanza kuangalia mazingira au hali zinazotuzunguka kwa wakati huo. Watu wakuu walishinda hofu zao kwa kuwa ndani yao walijua picha walionayo ndani ya mioyo yao ni halisi kuliko mazingira yao na tena imani yao haikuwa kwenye ahadi walizopewa bali imani zao waliziweka kwa Mtoa Ahadi.
“Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutoamini, bali alitiwa nguvu katika imani,Akimtukuza Mungu. Huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi” Warumi 4:20-21 (msisitizo umeongezwa)
Vita kubwa ya adui ni kutushawishi tusiamini na tutilie mashaka (doubt) juu ya kile ambacho Mungu amesema katika Neno lake kuhusu maisha yetu; kuamini kuwa unao uwezo ambao Mungu amesema unao; ya kuwa unaweza kufanya mambo ambayo Mungu amesema unaweza kufanya; unaweza kupata mambo ambayo Mungu amesema utapata amba kuwa Mungu anaweza kufanya yale aliyoahidi.
Kukosekana kwa imani huipa hofu nafasi ya kukua, kuongezeka kwa mizizi yake ndani yetu, hata kuwa mikubwa kiasi cha kutuzuia kufikia matarajio na mipango yetu ya kila siku; Pale tunapoanza kuamini uongo tu; ndipo uongo huo huanza kuwa dhahiri (manifested) katika maisha yetu (Ayubu3:25-26). Muamini Mungu, kuwa anaweza kutekeleza kile alichosema, na hakika atatekeleza kwa maana Yeye ni Kweli hakuna uongo katika maneno yake! Mtu mmoja amewahi kusema, “Usitie shaka kumuamini Mungu anayejulikana; kwa ajili ya mambo yasiyojulikana”

Tujifunze kwa Joshua na Kalebu.

Kuujua ukweli huu utakupa fursa ya kuishi maisha yenye ujasiri utakao itupa mbali hofu yako. Neno la Mungu na maono (vision) uliyonayo yanakupa uhakika na ujasiri kwamba, haijalishi mazingira uliyopo sasa, jambo hilo au mazingira hayo ni kwa muda tu kwa kuwa Aliyeahidi hakika atatimiza alichoahidi. Kama mazingira uliyopo hayafanani na picha ya mafanikio iliyopo ndani yako, usitie shaka upo hapo kwa muda tu.
Kama ndani yako unaona picha (vision) unamiliki kampuni yako mwenye yenye lengo la kuboresha maisha ya wengi na kumletea Mungu utukufu, basi mazingira yako ya sasa kwamba umeajiriwa au huna hata ajira yasikutie hofu ya kutokufikia picha hiyo. Kile usichokuwa nacho leo utakuwa nacho kesho, endapo tu utasonga mbele kuelekea picha hiyo bila ya kusikiliza kelele zinazopigwa na hofu.
“Wakati wewe unaogopa kufanya upendalo ili kutimiza ndoto zako, wenzako wanaogopa kuogopa na hivyo wanafanya”
Wewe pia ukimhesabu Mungu kuwa mwaminifu utashinda, hauna sababu ya kuogopa, kama iko sababu ambai ya kuogopa hofu yako (to fear your fear). Wakati wewe unaogopa kufanya upendalo ili kutimiza ndoto zako, wenzako wanaogopa kuogopa na hivyo wanafanya. Sababu moja wapo inayofanya tumwite Mungu katika sala ni ili kuondoa hofu zetu, tunapoomba tunakuwa jasiri kama amba na hapo tunafanya hata kupita tuwazavyo. Daudi anasema, “Nalimtafuta BWANA akanijibu, Akaniponya na hofu zangu zote” Zaburi 34:4!
Hiki ndicho kilichowapa nguvu Joshua na Kalebu, waiijua ahadi ya Mungu; ndani yao walikuwa na picha ya nchi mpya baada ya kuishi katika utumwa kwa muda mrefu. Neno la Mungu na picha ya maono waliyokuwa nayo, iliwapa ujasiri wa kusonga mbele hata pale walipokuta na mazingira ya kuwatia hofu. Kila walipokutana na changamoto katika kufikia kilele cha mafanikio yao jambo moja walizingatia, nalo ni kwamba, aliyeahidi ni Mwaminifu na Hakika Atatimiza Alichoahidi. (Hesabu 13:30-31, 14:24)
See you at the top…!

0 comments :