Unataka kufanikiwa katika nini?

1:00:00 PM Unknown 0 Comments


UNATAKA KUFANIKIWA KATIKA NINI?
“Success is predictable, so is the failure”
Nakubaliana na mwenyehekima mmoja aliyesema, “Success is predictable, so is the failure” (“Kufanikiwa au kutofanikiwa ni jambo la kutabirika”: Tafasiri isiyo rasmi). Kwa lugha rahisi ni kwamba mtu anaweza kujua kama atafanikiwa au hatofanikiwa katika maisha yake au katika jambo fulani kabla hata hajaanza safari. Mara nyingi nmeandika kuwa “Mafanikio katika jambo lolote kwenye maisha ya mtu si jambo la bahati nasibu; mafanikio huja baada ya kufuata na kutekeleza kanuni muhimu katika maisha ya mtu”. Na hiki ndicho kinachofanya mafaniko katika eneo lolote kuwa ya kutabirika (predictable) kwa kuwa mafanikio yamefungwa ndani ya kanuni (universal principles/laws).
“I always knew I was going to be rich. I don’t think I ever doubted it for a minute.” - Warren Buffett
(“Siku zote nilijua kuwa, nitakuwa tajiri. Sidhani kama nimewahi kuwa na shaka juu ya hili hata kwa dakika moja”: Tafasiri isiyo rasmi)
Kiwango cha mafanikio ya mtu katike eneo fulani hutegemea kiwango chake cha maarifa na ufahamu juu ya kanuni za mafanikio katika eneo hilo; iwe kiroho, kimwili, kifedha au kiuchumi, familia, huduma n.k (Mithali24:3-5). Leo nataka tuangalie kanuni/mambo mawili:
a.    Ufasaha wa maeneo unayotaka kufanikiwa au mambo unayotaka kufanikisha (clarity of vision)
Maisha ya kila siku yanadai mtu awe na uwezo wa kujua kwa ufasaha (clarity) anataka afanikiwe katika jambo gani ili kuishi maisha yenye kuleta matokeo (productive / effective life). Je, umeshawahi kukaa chini na kujiuliza unataka kufanikiwa katika nini kwenye maisha yao? Au unataka kufanikisha nini katika muda wa kuwepo kwako hapa duniani? Nakushauri tafuta muda ujiulize na kupata majibu ya maswali hayo. Tunaishi katika ulimwengu ambao kila mtu anaonekana kuwa ‘bize’, lakini ni watu wachache wanaoweza kuonesha matunda au matokeo ya ‘ubize’ wao; kwa watu wengi hasa vijana, ni rahisi sana kuwa ‘bize’; lakini si rahisi kuonesha matunda ya ‘ubize’ wako. Kusema tu unataka ufanikiwe katika maisha haitoshi, lazima uwe ‘specific’ ili uweze kujipima na kujitathimini kulingana na muda.
b.   Iandike njozi hii
Mambo mengi yanadai umakini wetu, muda wetu na rasilimali zetu; ndio maana kama hatua ya kwanza, tunahitaji kutambua (Define clearly) maeneo au mambo tunayotaka kuyafanikisha na kuyaandika mambo hayo sehemu maalumu itakayokuwa rahisi kwa kuyaona mara kwa mara. Kutambua pekee haitoshi, jifunze kuandika mahali. Labda unataka kuandika kitabu au kuanzisha biashara au kuanzisha chanzo kipya cha mapato au mradi (project); hata kama mazingira hayafanani na kile unachotaka kufanikisha fuata ushauri aliopewa Habakuki, Iandike (Hab 2:2); unapoandika wazo lolote linakuwa wazi zaidi (clarified) ndani yako na inakupa hamasa na wepesi wa kuliendea. Kwa utafiti mdogo tu, asilimia kubwa ya watu waliofanikiwa katika maeneo mbalimbali; walikuwa na mawazo hayo ya vitu au mambo tunayoyaona kwao wakati huu kwenye maandishi, waliandika matamanio yao; waliyaona na kuyaandika kabla ya sisi kuyashuhudia...!
There’s a place for you at the top!

0 comments :

Jizoeze kuwekeza katika maarifa

12:49:00 PM Unknown 0 Comments

 
JIZOEZE KUWEKEZA KATIKA MAARIFA
"Until your brain sweat, you won't experience swiftness"
Katika kitabu cha Hosea 4:6 imeandikwa “watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa…” Inawezekana umesikia mara nyingi sehemu hii; swali ambalo nataka tujiulize kwa pamoja na kulitafakari ni, je kwanini Mungu hamzuii au hajamzuia muangamizaji wa watu wake? Kumbuka hawa wanauhusishwa hapa si wapagani bali ni watu wa Mungu; hivyo swali linabaki kwanini Mungu hajamzuia mwangamizaji na ameacha mpaka wanaangamizwa?
Isaya anandika, “Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa;...” Isa5:13. Hapa pia nataka tujiulize kwa pamoja, kwanini Mungu hakumzui mtekaji au watekaji  mpaka watu wake wanatekwa? Kwanini watu wake wanatekwa mbele yake na ameacha mpaka wamechukuliwa mateka?
Dr. David Oyedepo amewahi kusema, “God cannot help you and I beyond our level of knowledge of Him” yaani Mungu hataweza kutusaidia zaidi ya kiwango chetu cha maarifa (ufahamu) tulichonacho (Tafasiri isiyo rasmi). Mpaka umeujua na kuelewa ‘ukweli’ huu hauwezi kuelewa pale Mfalme Suleimani aliposema na kusisitiza juu ya kuwekeza katika maarifa na ufahamu, “Bora hekima, basi jipatie hekima; naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu (wisdom is supreme, therefore get wisdom; though it may cost all you have get understanding)”.Mith 4:7
Petro anasema, uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu VYOTE, lakini tunauwezo wa kuvifikia (experience in our lives) vitu hivyo kwa njia ya maarifa katika yeye (2Petro1:3, msisitizo umeongezwa). Kumbuka, Mpaka pale umejitoa kuwekeza katika maarifa na ufahamu katika eneo husika, hautaweza kubadili nafasi uliopo, iwe katika eneo la elimu, uchumi, biashara, uongozi, uhusiano, kazini.. N.k (Until you give yourself to the investment in knowledge and understanding, you won’t change your position)
Uwekezaji katika maarifa unahitaji uwekezaji wa muda, juhudi na rasilimali zingine ili kupata matokeo bora katika maisha yetu ya kila siku. Mpaka umewekeza katika maarifa, maisha yako yanabaki kuwa mawindo mepesi kwa muangamizaji na mtekaji. Ni ‘kweli’ ulioijua pekee katika eneo husika (specific) ndio itakayokufanya au kuwezesha kuishi huru katika eneo hilo. Yh 8:32! Kumbuka, maombi hayawezi kubadili sehemu ya maarifa; kama eneo hilo linahitaji maarifa ili uweze kuvuka, hata kama utafunga na kuomba bila maarifa hayo hauwezi kubadili mahali ulipo (Prayer cannot replace the role of understanding and knowledge)!
Mwenyehekima mmoja anasema, asilima kubwa ya changamoto alizonazo mtu majibu yake yapo kwenye vitabu na semina mbali mbali ambazo alikuwa na nafasi ya kuyafikia maarifa lakini hakufanya hivyo kwa sababu yoyote ile.
There’s a place for you at the top!

0 comments :

Weekend of purpose ya kesho

8:59:00 AM Unknown 0 Comments

 
WEEKEND OF PURPOSE YA KESHO
(Ni Jumamosi ya kesho 13/05/2017 kuanzia saa tatu asubuhi)
Ni zaidi ya miaka miwili sasa tangu Mungu atupe wazo la kufanya , “Weekend Of Purpose” wazo hili tulilipata kwa BWANA. Nyakati hizo baada ya kumaliza Chuo kikuu tulikuwa tunakutana Tegeta siku za weekend kwa ajili ya kubadilishana mawazo, kusali, na kutiana moyo katika harakati za muda huo na baadaye. Siku moja katika kuomba kwetu ndipo BWANA alipotusemesha kuhusu jambo hili nasi tukalitenda.
Tukaanza kuandaa “Weekend Of Purpose” ya msimu wa kwanza na hatimaye kesho itakuwa ya tano. Ni siku mbili ambazo Bwana Alituambia tuwafundishe watu makusudi ya kuumbwa kwao, kwamba anawajua na amewaumba kwa kusudi maalumu. Kazi yetu ni kukufanya ujue kusudi la kuumbwa kwako na kukukumbusha umuhimu wa kulitenda na kukupa mbinu za kulifanikisha pia. Yeremia 1:5
Siku ya mwisho, wako watakaojuta kwa nini hawakufanya hili na lile, na wako watakaofuraha na kusema, I am so glad I did! Raha ya kifo cha mtu wa Mungu ni kutimiza kusudi. Kifo cha mtu wa Mungu kinamfurahisha Mungu maana ni usingizi wa amani baada ya kazi. Ni faida kuu, kuishi kusudi uliloitiwa na BWANA. Kifo ni kitamu kazi yako ikiisha vizuri, kinyume na hapo ni janga. Zaburi 116:15
Tunazo shuhuda za waliohudhuria Weekend Of Purpose ya kwanza na baada ya kujua kusudi la kuumbwa kwao, waliacha yale yasiyo ya kwao na leo hii wanafuraha kwa sababu wanatumikia kile ambacho Mungu alitaka wafanye.
Jaribu kufikiri kama Petro angeendelea kuvua samaki milele, angetoa hesabu gani mbele za Mungu; ambaye kwa hakika hakumweka awe mvuvi wa samaki, bali awe mhubiri wa injili. Utajisikiaje siku hiyo Yesu akikwambia nilikuumba uwe nahodha wa meli ilhali wewe umeishi maisha yako yote kama daktari wa meno. Ni kazi yetu katika Weekend Of Purpose kukusaidia kujua karama na makusudi ya kuumbwa kwako. Mafundisho yatakusaidia umalize vizuri sana, Zaburi 116:15
Katika “Weekend Of Purpose” utajengwa kitabia kama mwenye hekima mmoja alivyosema, “iweni watakatifu kwanza ndipo muwe wamisionari” neno hili ni kwa kila kada, iweni watakatifu kwanza ndipo muwe madereva, iweni watakatifu kwanza ndipo muwe wahandisi, iweni watakatifu kwanza ndipo muwe wagavi. Utajengwa ili tabia yako ifanane na kazi yako na kusudi uliloitiwa. Mhasibu ukionekane katika taswira ya fundi makenika (fundi wa magari) akiwa gereji bila shaka utaambiwa rudi nyumbani kavae ki-hasibu. Tabia ni matendo na mazoea yanayohusu matamshi, mavazi, matendo na mwenendo wote.
Karibu sana kesho Jumamosi saa tatu, ukifika Mawasiliano au Makumbusho panda magari yaliyoandikwa Bunju/Tegeta au Bagamoyo shuka kituo kinaitwa CHAMA KWA MASISTA- pale BOKO, vuka barabara, elekea upande huo wa kuume wa kanisani mpaka utakapoona geti la Masista wa Karmeli ambalo liko mbele baada ya kumaliza uzio wa kanisa utakuwa umefika.
Hautajutia kufika ni faida tupu, tukutane hapo. Mungu akubariki.

0 comments :

10:58:00 AM Unknown 0 Comments

 
USIMDHARAU MSHINDANI WAKO.
(Don’t underestimate your rival)
Ikiwa mhitimu wa chuo kikuu ataambiwa ajiandae kwa mtihahi wa darasa la kwanza, nadhani maandalizi pekee atakayofanya ni kwenda kwenye huo mtihani ambao unaonekana ni wa chini sana ukilinganisha na kiwango chake cha elimu. Lakini ikiwa ataambiwa atafanya mtihani au unaofanana na elimu yake au zaidi bila shaka atajiandaa sana.
Mshindani wako au adui si lazima awe mtu inaweza ikawa ni hali fulani (situation/condition). Inaweza ikawa ni hali ya umasikini, hali ya ugonjwa, kutokukubalika au vinginevyo. Mshindani wako inawezekana ikawa ni tofauti ya mahali ulipo na pale unapotaka kwenda. Yote kwa yote ni lazima tujizatiti, taking this battle very serious!
Ukijua kwamba mpinzani wako ni mwepesi (si lazima awe mtu) unaweza kufanya maandalizi mepesi na ndio chanzo cha kuangamia kwako. Unadhani nini kinatokea kwa wanaojua kwamba, kesho watashindana na mwanadamu mwenye kasi zaidi yaani Usain Bolt? Si siri watajiandaa sana, wanajua mpambano ni wa kufa na kupona.
Nini kinatokea kwa mzungumzaji anapojua katika mjadala huo atakuwapo Rais mstaafu wa Marekani Barrack Obama pamoja na Baba Mtakatifu Papa Francis. Ni wazi mzungumzaji atajipanga vilivyo, nini aseme na nini asiseme. Ukijua utazungumza mbele ya TD Jakes lazima ujipange. Ukijua kwamba kesho utapambana na Mike Tyson (wakati wa zama zake) na hujajiandaa vizuri, naamini utaomba udhuru kuliko kuweka maisha yako rehani. Preparation is a key!
Maisha nayo yako hivyo tunapaswa kuyaendea kwa kujiandaa kufa na kupona. Ukiwa shuleni soma, kazini fanya kazi kwa bidii, katika biashara pia ni vizuri kuwa na weledi wa kutosha. Ukiyadharau maisha ukisema ndege wa angani wanakula, tutakusubiri tukuone na wewe kama utaruka kwa mbawa. Tutasubiri tuone kama na wewe utaingia kwenye mashamba ya watu bila kibali kama ndege.
Kufurahia maisha haina maana kutokujizatiti kufanya vizuri na kuishi hadhi ya juu. Si kila mwenye nguo yenye kiraka ni bahati mbaya, wengine wanapata malipo ya kazi yao. Wakati wenzao wanasoma wao walilala, wakati wenzao wananunua mashamba wao waliongeza mke wa pili, wakati wenzao wanakwenda mazoezini wao walikwenda kulewa pombe.
Usiyachukulie maisha haya kirahisi, chukua wajibu wa kuyapanga na kupangilia. Wapenda hadithi mnakumbuka hii, Sungura alipomtazama kobe alimchukulia kirahisi sana. Sungura alimdharau kobe akiona hawezi kushindana naye katika riadha, hii ilipelekea sungura kucheka sana kwa nini apambane na kobe. Mbio zilipoanza sungura alikimbia kwa kasi na alivyogeuka nyumba aliona kobe yuko pale pale, Sungura kwa dharau akaamua kulala. Hatimaye usingizi wa pono ukamkuta sungura, na hatimaye kobe akampita na kutwaa ushindi. Japo kobe alikuwa taratibu alikuwa akimaanisha kushindana na alikuwa amejizatiti kweli kweli. Somo, usiwe kama sungura, take this life very serious!
Tukutane Boko Karmeli kwa weekend of purpose timu nzima ya Life Minus Regret itakuwa pale kuinjilisha na kufundisha na kusisimua. Usikose siku hiyo moja tu,  itabadili kabisa maisha yako.

0 comments :