Kanunu ya Mazingira
KANUNI YA MAZINGIRA
(Vigezo lazima vikamilike)
Ili
mbegu iweze kuota ni lazima vigezo vinavyohusika vikamilike. Uoteshaji wa
mbegu hauhitaji maombi tena haufanyiki kwa mafungo bali kwa kutimiza vigezo
vinavyotakiwa katika kanuni ya mazingira. Ili mbegu ikue inahitaji yafuatayo:
maji, mwanga, joto na hewa. Mambo haya yakitimia hata kama mkulima ni mweusi
mbegu itaota na hata kama ni mweupe mbegu itaota. Ukitii na kutimiza vigezo
mafanikio ni lazima.
Kuna
watu ili wafanikiwe wanahitaji mazingira ya kanisani, wengine mazingira ya
biashara wengine mazingira ya shuleni na wengine viwandani. Yule wa kanisani
hawezi kuwika sokoni halikadhalika wa sokoni hawezi kuwika kanisani. Ni muhimu
kila mtu ajue mazingira yanayobeba kipaji chake. Mito na bahari ndiyo inayobeba
kipaji cha samaki cha kuogelea.
Unadhani
mazingira gani yanaweza kubeba kipaji chako? Je, ni katika mazingira gani watu
wanauona uwepo wako? Je, ni katika
tasnia gani unapata utoshelevu wa mahitaji yako? Ni katika mazingira gani Mungu
anatukuzwa kwa ajili yako na wewe unatakaswa?
Nimewahi
kusoma makala moja isemayo, tasnia ya filamu imeajiri watu wengi nchini Nigeria
kuliko mafuta. Ingawa Nigeria wanasifika kwa kutoa mafuta lakini ni mazingira
ya filamu ndiyo yamewaajiri watu wengi zaidi. Ni bora kupingwa na watu wengi
katika mazingira sahihi kuliko kukubaliwa na watu wote katika mazingira ambayo
si sahihi kwa ukuaji na ustawi wako.
Bora
upinzani wa jinamizi la usiku kuliko ule wa mazingira yaani, unaamka mapema
kwenda kufanya kitu usichopenda. Unawahi kuamka kwende katika mazingira
usiyoyataka. Kama umeitwa katika mazingira ya michezo basi siasa haikufai. Ni
raha sana mtu anapokuwa katika mazingira sahihi, Christiano Ronaldo anasema
yuko tayari kucheza soka hata bila ya kulipwa. Anaupenda mpira wa miguu, yuko
radhi kucheza bure mpira ni maisha yake. Usain Bolt angeendelea kung’ang’ana na
mpira wa miguu huenda asingekuwa chochote, lakini utii wake kwa kanuni ya
mazingira ulimpeleka kwenye riadha ambapo anashikilia rekodi ya dunia.
Mwenye
hekima mmoja amewahi kusema: “There are no bad people there are misplaced
people”. Hakuna watu wabaya ila kuna
watu ambao wapo katika mazingira ambayo si sahihi kwao. Mazingira mabaya si
yale yasiyo na pesa bali ni yale ambayo hayakusaidii kufikia ndoto zako na kuwa
unachotaka kuwa. Mazingira yanapaswa kukubeba kwa sababu kwa asili mtu hawezi
kubeba mazingira. Kuyabeba mazingira ni kazi ngumu. Ndio maana
Rai
yangu kwako leo ni kukusihi utii kanuni ya mazingira na kwenda kwenye eneo lako
husika. Wahubiri wengi wamekuwa na simulizi za kuacha kazi na kwenda kwenye
wito wao, jambo hilo si mtindo bali ni kanunu ya msingi ya mazingira.
Nenda
shule, nenda kwenye biashara, nenda kanisani, nenda kwenye huduma, nenda kwa
watoto, nenda kwa yatima nenda kwa watu ambao umeitiwa. Wengine wameitwa katika
mazingira ya ujasiliamali wengine wameitwa katika mazingira ya uongozi. Sote
tunapaswa kuyatafuta mazingira yetu na kuyatii. Petro alicha mazingira ya
baharini [uvuvi] na akaenda katika mazingira yenye watu wengi [kwenye
uinjilishaji na utumishi] huko akafanikiwa sana.
Tii
mazingira yako, ipende kanuni ya mazingira….
0 comments :