Yesu ni mwalimu mwema

12:19:00 PM Unknown 0 Comments

 
YESU NI MWALIMU MWEMA.
Tuyatii Maagizo Yake
Kijana mmoja tajiri alimwendea Yesu na kumwita, “mwalimu mwema” naye Yesu akitaka sana kumtukuza Baba wa Mbinguni akasema, “aliye mwema ni mmoja”. Kwa kawaida mtu anapokusifu au anapokupa heshima yako huonesha utii kwa nafasi yako. Katika dunia ya leo tunawasomi wanaoitwa daktari bigwa, Profesa, wako wahandisi hata marubani.
Kuwasifia wataalamu hawa pasipo kutekeleza wanachosema ni sawa na kufukuza upepo, ni kuwavisha kilemba cha ukoka. Kumwita mtu Daktari bingwa hakuleti maana ikiwa akikikushauri jambo lihusulo afya utakataa . Ni heri asiyemwita kwa cheo lakini akafuata maelekezo yake. Vivyo hivyo haileti maana tumwitapo Yesu mwalimu ilhali hatufuati asemalo. Ukimjua Yesu kama mwalimu mwema lazima ukubali kufanya asemalo hata kama kwa akili za kawaida linaonekana ni la ki-puuzi au ni la kuaibisha.
“Ukimjua Yesu kama mwalimu mwema lazima ukubali kufanya asemalo hata kama kwa akili za kawaida linaonekana ni la ki-puuzi au ni la kuaibisha”
“Na tazama, mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele? Akamwambia Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri. Akamwambia, Zipi? Yesu akasema, Ni hizi, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Yule kijana akamwambia, Haya yote nimeyashika; nimepungukiwa na nini tena?  Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate. Yule kijana alipolisikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.” Mathayo 19:17-22
Licha ya kumwita Yesu mwalimu mwema yaani, “Good Master” lakini kijana hakukubali ushauri wa Yesu. Alipoambiwa auze kila kitu na kuwapa masikini hakukubali. Anajua Yesu ni mwalimu mwema, anajua Yesu ni mtaalamu wa roho, mwili na nafisi za  wanadamu lakini hataki kumtii anachosema. Alijua Yesu ni kila kitu lakini hakutaka kumsikia. Wako wengi wanamwita Yesu Bwana, wengine wanasema, “nakupenda Yesu” lakini hawataki kutii neno lake. Yeye mwenyewe anasema, “mkinipenda mtalishika neno langu”
Naamani Yule Jemedari anafanana na huyu kijana tajiri. Yeye alipokwenda kwa Elisha nabii hakutaka kujichovya mtoni mara saba. Alitaka Elisha amwekee mkono. Mara nyingi tunapokwenda mbele za Mungu tunakosea, tunakwenda kumwagiza badala ya kwenda kumsikiliza. Mungu anaweza asiseme na wewe kwa njozi, wala kwa nabii wala kwa dalili. Lakini kupitia neno lake (Biblia) anasema nasi kila siku. Kila tunaposoma maandiko tunasikia sauti ya Mungu. Biblia ni redio yake, isome na usikilize. Naamani hakutaka kusikia maagizo ya nabii bali alitaka nabii ndiye afuate mawazo na maagizo yake. Lakini Naamani akakasirika, akaondoka, akasema, Tazama, nalidhania, Bila shaka atatoka kwangu, na kusimama, na kuomba kwa jina la Bwana, Mungu wake, na kupitisha mkono wake mahali penye ugonjwa, na kuniponya mimi mwenye ukoma.”2 Wafalme 5:11
Jambo zuri ni kwamba, kijana tajiri alimuuliza Yesu swali ambalo kila mwenye akili timamu anapaswa kujiuliza. Mtu mzima hapaswi kujiuliza maswali ya kisiasi tu, bali anapaswa kujiuliza maswali yahusuyo umilele wake na watoto wake. Kijana akamuuliza Yesu, “nifanye nini ili nirithi uzima wa milele?”. Hakuuliza kwa habari ya Simba na Yanga, wala hakuuliza kwa habari ya CHADEMA na CCM, hakugusa habari za kuoa na kuolewa wala hakuhoji kwa habari ya Manchester United na Arsenal bali alihoji kuhusu uzima wa milele. Kwa hili ninampongeza. Kila mwenye hekima ni lazima ajue atakuwa wapi baada ya kifo. Swali hili linapaswa kutawala akili ya kila mwanadamu. Uzima wa milele! Uzima wa milele! Uzima wa milele!
“Si vibaya kumiliki pesa, lakini ni hatari kama pesa zitatumiliki sisi hata tushindwe kumpa Mungu nafasi ya kwanza””
Yesu akimjibu Yule kijana alimwambia akitaka uzima wa milele azishike amri, wewe na mimi pia tukitaka uzima wa milele ni muhimu tuzishike amri zake Mungu. Si vibaya kumiliki pesa, lakini ni hatari kama pesa zitatumiliki sisi hata tushindwe kumpa Mungu nafasi ya kwanza. Yule kijana aliiona ni heri akose ukamilifu lakini abakie na pesa. Aliona bora akose furaha lakini abakie na pesa. Aliondoka kwa huzuni, watu wengi wana pesa lakini hawana furaha ya kweli, mali zao zimewatenga na ukamilifu.
Uzima wa milele unapatika kwa kumwamini BWANA YESU. Tena kila aliaminiye jina lake anao uzima wa milele. Ukimwamini leo na kuisikia sauti yake utaokoka. Usimwite BWANA kama hutaki kufanya aliyokuamuru yaani, kushika amri zake. 
Siku ya mwisho Yesu atawaita mashahidi wawili, ataliita neno lake na kupima utii wetu kwa neno lake. Agano jipya ni shahidi wa pili na Agano la kale ni shahidi kwanza. Mashahidi hawa wawili watapima utendaji wetu wa neno. Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili,”Ufunuo 11:3a

0 comments :

Baada ya kulitambua kusudi la kuumbwa kwako

9:23:00 AM Unknown 0 Comments



BAADA YA KULITAMBUA KUSUDI LA KUUMBWA KWAKO
Ukishafikia hatua ya kutambua kusudi la Mungu juu ya maisha yako hatua zifuatazo ni muhimu sana:
  1. Liandike
Ni muhimu sana kila mtu kuandika kusudi lake au maono yake katika aya yenye sentensi chache iwezekanavyo. Hii itakusaidia kulikumbuka daima kila unapoona sentensi hiyo na kukupa nguvu ya kuiendea hadi mwisho [Habakuki2:2—3].
“Ni vizuri kuibandika karatasi hiyo inayoelezea picha ya maono ya maisha yako ya baadae [kwa ufupi], chumbani au mahali popote pa wazi ili kila uisomapo uweze kukumbusha na kukuhamasisha”
Nimewahi kusoma mwandishi mmoja ambaye yeye anashauri sentensi  hizo zisizidi tatu, lakini kwa maoni yangu si mbaya hata zikifika tano. Tazama kusudi la Yohana mbatizaji lilivyo katika sentensi chache.Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana. Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeyeYohana 1:6
Ni vizuri kuibandika karatasi hiyo inayoelezea picha ya maono ya maisha yako ya baadae [kwa ufupi], chumbani au mahali popote pa wazi ili kila uisomapo uweze kukumbusha na kukuhamasisha. Kwa mfano zifuatazo ni sentensi ambazo nimeandika ili kuelezea kusudi la kuumbwa kwa watu kadhaa ukianza na mimi:
1.      “My purpose is to you use all I have, to give myself into the preaching of the gospel and inspire others to live for Christ” Alphonce Luhamba’s vision (purpose) statement
2.     “To uplift humanity consciousness through business”
3.     “To inspire and empower people to live their highest vision in context of love and joy”
4.     “To create and inspire one million millionaires who each will donate one million dollar to his or her church charity”
Ni vema kurahisisha kwa kuandika au kuchora alama zenye kuonesha picha ya kusudi la kuumbwa kwako. Mchoro huo au maneno hayo ni lazima yawe yanakuvutia, yaweze kukuhamasisha na kukupa changamoto ya kuyafanyia kazi katika kutimiza kusudi hilo.  [Your Vision or purpose paragraph must challenge your comfort zone.]
Ni vizuri kulisoma kusudi lako kila siku, ni vema kuliacha liimbe kichwani mwako kila dakika. Kama Ilivyokuwa kwa Yohana mbatizaji wewe pia umetumwa na Mungu, na umetoka kwa Mungu. Haupo duniani kitalii, upo kikazi. Muda wote tuwapo duniani tupo safarini kwa kazi maalumu. Badala ya Yohana, waweza kuweka jina lako. Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake.....Yohana 1:6
  1. Achana na utafiti.
Ukishajua kusudi au maono yako haunabudi kuacha kujiuliza uliza maswali mengi. Hakuna haja ya kuogopa. Ni muhimu kudumu katika Neno la Mungu ambalo ndio chakula muhimu kwa kila mbeba maono na makusudi ya Mungu. Kusudi lako litaendana na Neno la Mungu hivyo usiache kulisoma.
“Kuachana na utafiti usio na tija kutakujengea ujasiri na uhakika wa kupata ushindi; na matokeo yake Imani yako kwa Mungu juu ya maono hayo itaongezeka”
Katika kusudi ushindi lazima. Kuachana na utafiti usio na tija kutakujengea ujasiri na uhakika wa kupata ushindi; na matokeo yake Imani yako kwa Mungu juu ya maono hayo itaongezeka. Achana na maswali ya nitaweza au sitaweza, Mungu aliyekuita atakuwezesha. Tunapokuwa katika kusudi la Mungu tuna uhakika na ushindi wala hatubahatishi.
Baada ya kuachana na maswali, unapaswa kubaki na maneno machache tu ya ushindi. “Nitaweza na nitafanya na nitakuwa vile ambavyo Mungu anataka niwe. Unapaswa kusema kama Daudi, Sitakufa mimi bali nitaishi, ili kufanya kazi niliyoitiwa na BWANA.
  1. Litende na kuimaliza kazi kwa gharama yoyote ile.
Kwa sababu ya hofu ya kulipa gharama mara kadhaa utajikuta katika nafasi ambayo ni rahisi kufanya kila kitu isipokuwa kusudi la kuumbwa kwako, hata hivyo unapaswa kulichagua kusudi lako hata kwa mateso. “Chakula change ndicho hiki niyatende mapenzi yake yeye aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake…”Yohana4:34. Jim Rohn anaandika, “Kama una nia ya kutaka kufanya jambo, utatafuta njia ili kulifanya; kama huna nia, utatafuta visingizio kwanini hauwezi kufanya” (Tafasiri isiyo rasmi)
Gharama inaweza kubwa lakini ni muhimu kuhakikisha kwamba kusudi linatendeka, maana gharama huakisi uzuri wa taji yako. Gharama inawezakuwa ya juu (steeper) kama vile: Kuacha kazi fulani, kurudi tena shule au kutengwa, kujikatalia mambo ya kidunia, kuonekana mshamba au kukosa muda wa kupumzika. Kusudi la Yesu lilimnyima hata muda wa kulaza ubavu wake. Ili kufanikisha jambo lenye kuleta maana duniani mwenye hekima mmoja anaandika, “Hakikisha kazi inafanyika kwa gharama yoyote”.
  1. Weka na kupanga  mipango
Maono au mipango ni ulinzi wako. Hatuhitaji “body guard” kama Rais, tunahitaji maono ili kutuokoka katika maangamizi. Mipango mizuri ya baadaye ni ulinzi tosha, itakuzuia na itakuruhusu pia. Pasipo maono na mipango dhabiti, watu huacha kujizuia na hivyo huangamia.
Mipango ni njia ya kuiendee hatima yako. Mipango ni hatua kuelekea katika hatima iliyowekwa mbele yako kwa sura ya maono [Mithali 16:9]. Ni vizuri mipango yako ikazingatia muda. Usikubali  kubahatisha au kupangiwa na mtu. Ni vizuri ukaweka mipango dhabiti ili kutekeleza kusudi la Mungu katika maisha yako. Mipango inakufanya uone mbele, inakusaidia usirejee nyuma. Mipango inakupatia nafasi ya kuishi maisha ulikwisha yafikiri. Pasipo mipango au maono watu hurejea nyuma na hivyo huangamia.
“Watu wanaopenda kufuata mkumbo hawapendi kupanga mipango yao wenyewe, wanaridhika kuwa mashabiki wa watu fulani au wa kikundi fulani”
Ukiwaruhusu watu wapange kwa ajili yako watakupangia kijisehemu kidogo; tofauti na wito au uwezo ambao Mungu ameweka ndani.  Mipango ni wajibu wako binafsi usioweza kukaimishwa [delegate] kwa mtu yeyote. Watu wanaopenda kufuata mkumbo hawapendi kupanga mipango yao wenyewe, wanaridhika kuwa mashabiki wa watu fulani au wa kikundi fulani. Usipopanga mipango yako, utaangukia katika mipango ya mtu mwingine; hii haikupi uhakika wa kufikia kilele cha mafanikio yako.  
“Utahitaji kuchochea kipawa chako; na hapa ni muhimu utafute maarifa na ujuzi sahihi ili kukuwezesha kutumia vyema kipawa chako”
  1. Tafuta maarifa
Wakati mwingine kusudi lako linaweza kukuhitaji utafute maarifa na weledi wa juu ili kulitekeleza kwa ufanisi.  Utahitaji kutoka kwenye “kipawa [gift/talent]” mpaka kwenye “ujuzi [Skills]”. Utahitaji kuchochea kipawa chako; na hapa ni muhimu utafute maarifa na ujuzi sahihi ili kukuwezesha kutumia vyema kipawa chako. Waweza kwenda shule ya muziki, au utahitaji kwenda shule ya sheria, au kurudi tena shule hata kama mwanzoni uliishia njiani, waweza kwenda shule ya Biblia ikibidi, waweza kuwa mfuasi wa mtu mwaminifu aliyefanikiwa katika eneo unalotaka kufanikiwa ili kujifunza kutoka kwake [mentorship/coaching].
Watu wengi wenye vipawa hufanana lakini juhudi, ujuzi na maarifa hufanya watofautiane; inawezekana wote ni waimbaji, lakini mmoja anaimba kwa ujuzi [skills] na mwingine hana ujuzi huo. Marafiki sahihi, usomaji wa vitabu na utazamaji wa vipindi vinavyolisha maono yako ni mambo yenye kukupatia msaada na kulifanya kusudi lako litendeke kirahisi, kwa ufanisi na kwa mafanikio makubwa.

0 comments :

Umuhimu wa kutambua kusudi - II

3:43:00 PM Unknown 0 Comments


UMUHIMU WA KUTAMBUA KUSUDI-II
Tofauti kati ya Kusudi (Purpose) na Maono (Vision)

Kusudi maana yake ni sababu iliyofanya au inayofanya kilichopo kiwepo au kitengenezwe jinsi kilivyo (design) ili kutimiza kazi maalumu; katika kufikia malengo yaliyokuwa yamekusudiwa awali kabla ya kitu hicho kuwepo au kutengenezwa.

0 comments :